Rais Samia ashiriki Hafla ya Kupokea Fedha za Msaada wa Bajeti ya Serikali kutoka EU, leo Julai 4, 2023

DP world wakiwekeza bandari itachangia 67% ya bajeti badala 30+ za Sasa,gesi ya Lindi ikianza itachangia 6tr kwa mwaka,ukombozi toka kwa mabeberu hauwezi kua wa usiku mmoja
 
Ajisikii hata aibu🤔🤔 miaka zaidi ya 60 ya uhuru bado mtawala anapata ujasiri wa kwenda kupokea misaada tuu 🤔🤔🤔 kulikua na maana gani ya kumuondoa mkoloni 🤔🤔si bora mkoloni angebaki tuu, Kila siku Wana mrudisha kwa mlango wa nyuma🤔🤔 amaa kweli bongo bahati mbaya🚶🚶🚶🚶
 
Still uvccm na walinda legacy wanawaita mabeberu 🤣🤣🤣 while mpaka budget ya Nchi mabeberu ndio wanasapoti miaka yote!!
 
[emoji90][emoji90][emoji90][emoji90][emoji90][emoji90]
 
 

Attachments

  • IMG_1035.MP4
    13.1 MB
Kupokea Fedha za Msaada wa Bajeti ya Serikali kutoka Umoja wa Ulaya (EU)

04 July 2023
Dodoma, Tanzania

Tanzania imesaini mikataba na Umoja wa Ulaya ya kiasi cha Shs. 455 bilioni


Serikali ya Tanzania imesaini mikataba mitatu na Umoja wa Ulaya yenye thamani ya zaidi ya Shs. 455 bilioni kwa lengo la kusaidia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka mpya wa fedha wa 2023/2024.

Mikataba hiyo ni pamoja na ule wa kuimarisha uchumi wa buluu na kuleta mabadiliko ya tabia ya nchi wenye thamani ya Shs. 279.2 bilioni, kuimarisha mifumo ya fedha ya Serikali na kuleta maendeleo kwa sekta binafsi wenye thamani ya Shs 160.79 bilioni.

Pia upo wa kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya wenye thamani ya Shs. 15.23 bilioni.

Akizungumza leo siku ya jumanne Julai 4, 2023 katika hafla ya utiaji saini mikataba hiyo iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza Tanzania kuendeleza ushirikiano na nchi za Ulaya uliodumu kwa zaidi ya miaka 48 sasa. Amesema msaada huo wa fedha utakwenda kusaidia maeneo muhimu ya utekelezaji wa bajeti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…