Ni mpango unaoenda kufeli sio muda mrefu.
Ungekuwa na chances kubwa ya mafanikio iwapo hayo mashamba anapewa mtu mmoja mmoja. Au serikali ina kitengo cha management ya hayo mashamba na kuyasimamia.!
Wazungu washajaribu hayo mambo kwenye up until 1800’s, shida ikaja wengine wavivu kutunza ardhi zao, mifugo inaingia kiholela, wengine awataki kuchangia miundombinu na mambo mengine luluki ya ovyo ikabidi hizo ardhi wakulima wadogo wanyan’ganywe na kupewa wakulima wakubwa.
Njia pekee ya kukuza kilimo ni kutaka watu kama kina Sumry yule aliekuwa na mabasi sasa kaamia kulima Rukwa, kuwa wengi nchi nzima, wenye uwezo wa kupanda na kuvuna kwa machines hekari kubwa.
Kutangaza sera zilizopo nzuri tayari kwenye kilimo sema wenye kuzielewa faida zake kwa kina ni wachache ili kuvutia uwekezaji. Kwa sasa kama una hela ya kununua mabasi 100 kwa mkupuo na kuacha kilimo wewe ni poyoyo ambae uelewi incentives za machinery zinazotolewa shambani.
Serikali ijikite na kutengeneza sera nzuri za kuvutia viwanda na miundombinu ya uwekezaji kwa sasa kama ilivyo kwenye kilimo.
Lakini huo mradi sio sustainable ni swala la muda tu, kikundi hakina ata leadership unaokota tu watu, soon kutakuwa na clashes of personality.
Huko maofisini kwenye management inayoeleweka kuimarisha team working bado kila mara HR wana implement theories za watu kama ‘Meredith Belbin’ ili kuimarisha ufanisi wa team; we ukaokote watu wafanyekazi kwa pamoja bila ya mgawanyiko wa majukumu wala uongozi humo ndani migogoro aipo mbali; worst makundi yote yanajukumu la pamoja kuhifadhi miundombinu ya umwagiliaji it will never work miaka 800.
Mpeni huyo Bashe wizara ya size yake, ukisikilizia anavyoongea utadhani mtu wa maana, kumbe ujinga mtupu. Ni waste of tax payers money.
Just google ‘why feudal farming failed in Europe au middle ages’ utapata picha kwanini wanzungu walifuta ujinga huu wa kuwapa watu ardhi ovyo na ku encourage large scale farmers: such schemes weren’t sustainable.