Rais Samia ashiriki Halfa ya Utoaji Tuzo za Wasanii wa Uchekeshaji Tanzania. Na kupewa tuzo ya Champion of Comedy

Rais Samia ashiriki Halfa ya Utoaji Tuzo za Wasanii wa Uchekeshaji Tanzania. Na kupewa tuzo ya Champion of Comedy

Yohana mbatizajii mwenzio alikuwa anakula nzige na asalii anakaa nyikani, wewe sijui unakula Nini mpaka unataka kukwaza tu watu 😂😂😂
 
Stop reasoning like class 3 dropout,Idiot
Don't expect anything significant from CCM whose party members have mouth diarrhea just like this Idiot
 
Stop reasoning like class 3 dropout,Idiot
Don't expect anything significant from CCM whose party members have mouth diarrhea just like this Idiot
Mzee nataka niwe naongea kingleza kama Cha kwako! Umesomea wapi? Wivu haujengi Mzee, kuliko kukuonea wivu Bora niwe mkweli unisaidie na Mimi nijue kingleza
 
Makongoro ndiye mtoto mtoto halisi wa Mwalimu Nyerere sio hawa imposters Steve na Yericko.
 
Rais Samia akishiriki Halfa ya Utoaji Tuzo za Wasanii wa Uchekeshaji Tanzania Ukumbi wa The Super Dome Februari 22, Dar es Salaam.

Pia soma: Pre GE2025 - Rais Samia kuwa mgeni rasmi wa kwenye tuzo za Tanzania Comedy Awards

Updates....
- Rais Samia apewa tuzo ya Champion of Comedy; nami nasema anafaa

-Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ameshinda tuzo ya Kiongozi Mcheshi katika Usiku wa Tuzo za Ucheshi (TCA) Zilizofanyika katika Ukumbi wa Super Dome Jijini Dar es salaam.

Katika Kinyanganyiro hicho Makongoro alikuwa akichuana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, Mchingaji Hananja, Mkuu wa Mkoa Mstaafu Aggrey Mwanri na Sheikh Kipozeo.

-Wachekeshaji Steve Mweusi na Ndaro wameibuka washindi katika kipengele cha Best Comedy Duo katika tuzo za wachekeshaji Tanzania.

-Mchekeshaji maarufu Bongo, TX Dullah ameibuka mshindi katika kipengele cha Best Male Digital Comedian of The Year (Mchekeshaji Bora wa Kiume wa Kidijitali wa Mwaka) katika Tuzo za Wachekeshaji Bongo.

-Leonardo ameibuka Mshindi wa Jumla akinyakua Tuzo kubwa ya Overall best comedian of the year kwa wanaume na wanawake.

-Mama Mawigia ameshinda Tuzo ya Best Female Digital Comedy of the Year leo Februari 22, 2025 jijini Dar es Salaam.

-Msanii wa Muziki, Omary Nyembo maarufu Ommy Dimpoz amesema kuanzia siku ya leo Februari 22, 2025, wachekeshaji (comedians) wa Tanzania, hashtag yao ni "Cheka na Samia" na popote alipo Rais Samia Suluhu Hassan nao wapo!

"Kwa hiyo, sisi wenyewe kwa kufurahi na kufurahishwa na uwepo wa Mheshimiwa Rais (Samia Suluhu Hassan), leo tukasema kuanzia leo tutaita wachekeshaji wote kuhakikishia kwamba tunamsapoti Rais na tutaenda kama 'Cheka na Samia'.

- Eliud Samwel amenyakua tuzo ya mchekeshaji bora wa jukwaani maarufu kama Stand Up Comedy.

- Lucas Mhuvile, maarufu kama Joti, ameshinda tuzo ya The Best Actor Comedian of The Year

- Dogo Sele amepokea tuzo ya mwaka 2025 kama mchekeshaji bora mtoto

- Neyla Manga Amechukua Tuzo ya Mchekeshaji Bora wa Kike wa Jukwaani kwa mwaka 2025.

-Familia ya marehemu King Majuto imepokea tuzo ya heshima katika Tanzania Comedy Awards, ikitambua mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya vichekesho

Katika hali ya utani, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema wazo lililotolewa na wachekeshaji la kucheza mchezo wa ‘upatu’ linaweza kuwa zuri endapo likibadilishwa na kutafutiwa namna bora ili kusaidia masuala ya kifedha ya nchi za Kiafrika.

Rais Samia amesema wazo hilo likichukuliwa kitofauti litakuwa na mchango wa kujitegemea kifedha, kama wakikubaliana na viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuunda mfuko wao.





Kwa hiyo Saa 100 ndiye mchekeshaji mkuu wa Taifa!? Ndio maana mambo yanajiendea tu kama wakati wa yyle Vasco Da Gama wa Msoga Chalinze!
 
Nampa pongezi sana Rais kwa kupata tuzo ya Ubingwa wa Kuchekesha. Ni wazi akina Joti na Nanga wamekuwa wakimfuatilia kwa makini na kung'amua kipaji alicho nacho.

Sasa ni watu gani pia wanapaswa kuja mtunuku Cheti kingine ndugu Rais?
 
Hivi sisi madalali na mawinga na sisi tunaruhusiwa kutoa tunzo??
Nyie ni wafanyabiashara, nishawahi kuwa winga baadae dalali wa simu na magari, ni mfanyabiashara.

Alafu kumjibu mtoa mada. Hiyo tuzo iliitwa Champion of comedy unaweza usijue kwa kiswahili, kwa muktadha wake tunamuita mlezi au mwanaharakati wa ucheshu. Amechampion amewezesha tuzo hizo kuwepo. Ila si ulivyosema umeamua kuwa sarcast.
 
Back
Top Bottom