Leo ni kumbukumbu ya Uhuru wa Taifa la Ufaransa, nipo naangalia Live. Rais Macron ndiye Mgeni rasmi, pia kuna ugeni wa nchi nyingi za Ulaya. Kilichonivutia ni security coverage ya wenzetu wazungu.
Gari ya Rais imefika kisha askari Polisi akamfungulia mlango hapakuwa na mtu mwingine pale, kisha Rais akatembea peke yake kuelekea waliposimama wakuu wa vyombo vya majeshi na kusalimiana nao.
kisha akaongozana na mkuu wa Majeshi peke yao kupanda gari la wazi( mita kama 50, pale gari la wazi hapakuwa na mtu mwingine zaidi ya dereva tu, gari likaondoka wakiwa wamesimama wawili tu na nyuma kukiwa na pikipiki za Polisi kama 20 hivi.
Kisha alipofika kwenye uwanja wakashuka kisha Rais peke yake akaelekea kukagua gwaride kisha kuelekea jukwaani. Yaani pamoja na kuwa na watu wengi sana lakini sikuona Askari wakiwa pembeni na kuambatana naye na mabunduki makubwa, wala sikuona suti nyeusi hata mmoja au wakiwa wamening'inia kwenye milango ya gari nyuma ya gari ya rais.
Kiuhalisia gwaride likiwa na mchanganyiko wa mavazi huwa halipendizi mfano kukuta watu wamevaa kiraia halafu wanapita kwenye gwaride, inaleta maana sana kukuta aliyevaa kiraia(suti) ni rais peke yake. Maoni yangu kama ni suala la kiusalama ni vema ifanyike utaratibu kwa walinzi wanaoingia na rais wavae kijeshi ili isiharibu muonekano wa gwaride.
KITENGO Mnapiga kazi nzuri sana iliyotukuka lakini hebu jaribuni Kwenda Mbali zaidi na kuchukuwa mengine ya wenzetu yatakayofaa ktk mazingira ya kwetu. Nadhani pia hii ya Ufaransa huenda wamezingatia shughuli inafanyikia wapi, lakini KWETU TZ NA AFRICA DAAAAAH!!! Sisi Africa unakuta coverage haitofautishi hapa ni Kibiti na hapa ni parokiani.
Mkipata muda jaribuni kuangalia Maadhimisho ya kumbukumbu ya Uhuru wa Ufaransa iliyofanyika leo kuna kikubwa mtajifunza tu