Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Juni 27, 2022

Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 25 ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote, Juni 27, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Sherehe ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Fursa sawa kwa wote (Silver Jubilee of Equal Opportunities for All Trust Fund - EOTF ) katika Ukumbi wa JNICC - Dar es Salaam leo tarehe 27 Juni, 2022.




Rais Samia ameanza kuzungumza, ameanza kwa kutoa salaam na Shukrani kwa viongozi na makundi mbalimbali waliohudhuria tukio hili.

Hotuba ya Rais Samia
Rais samia:
Kwanza kabisa nianze kumshukuru Mungu kutujaalia kukutana hapa kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya mfuko wa fursa sawa kwa mote. Shukrani zangu zaidi ni kwa Mwenyekiti wa Mfuko na Bodi ya Wadhamini kwa kunialika leo hii kuja kushuhudia miaka 25 ya EOTF

Rais Samia: Shukrani kwa EOTF kwa kuibua vipaji vya wengi, hapa kuna watu wametoa ushuhuda nami nataka nitoe wangu. Mimi mwenzenu nilijiunga na EOTF ule ule mwaka iliyonzishwa 1997 nikiwa kama moja ya bodi ya wadhamini kijana kisichana machachari sana.

Rais Samia: Nilifanya kazi pamoja na Bodi na nilienda kwa miaka mitatu/ minne mpaka mwaka 2000 nikaingia mambo ya siasa na iliyoniingiza siasa ni EOTF.

Rais Samia: Nakumbuka siku moja tulikwenda kuwatembelea wakina Rigimbana kijijini kwao kule. Rugimbana naye ni mfaidika wa EOTF. Nilipokuwa kijijini magari yalitaka kuniacha. Mama wa Rais akanipandisha ndani ya gari lake.

Rais Samia: Akiwa ndani ya gari lake aliniambia mambo yafuatayo: Samia nimekuona tangu ulivyojua, nimekuona namna unavyokwenda na unavyofanya. Wewe ni Mwanasiasa mzuri sana. Sasa uchaguzi unaokuja ungejaribu kuingia. Niamwambia mama sijui watu wanaingiaje huko, akajibu we uliza uliza tu huko kwenu Pemba utaingia.

Rais Samia: Nafikiri aliniambia maneno haya mwaka 1999 kuelekea 2000 lakini maneno yale yakawa kichwani nikajiuliza ntaanza wapi. Lakini niasema ntajaribu mandari mama amesema. Kwahiyo nakaenda kuulizia kuingia inakuaje, lakini upande mwingine nilikuwa nakerwa na majibu yanayotoka ndani ya Baraza la Wawakilishi.

Rais Samia: Nikasema nadhani mama kaniambia niende kule nadhani kule ndiyo kwenye kazi yangu, basi nikajaribu, nilipojaribu nikashikwa mkono vizuri nikaingia nikawa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na safari ikaanza hapo. Moja kwa moja Waziri, nikaingia tena Waziri, nimegombea tena Mgombea Mwenza safari imenifikisha hapa. Lakini nguvu ya kuingia imetokana na Mama Mkapa. Wapo wengi ambao tumejengewa uwezo na EOTF.

Rais Samia: Kabla sijaingia kwenye ukumbi huu nilipata fursa ya kuangalia bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na vikundi vya wanawake. Wanawake wengi wananiambia mimi niko na EOTF mwaka 23 wengine 24. Kwahiyo nipongeze kwamba Mama ameweza kukaa na Wanawake muda wote huo akawalea kutoka tulipoanza na leo walipofika ni kazi kubwa sana.

Rais Saamia: Nimefarikika kuona mwamko wa wanawake na vijana ambao ndio walengwa wa Mfuko huu wa EOTF. Nimefarijika kuona mlivyojituma katika kuendeleza maisha yenu, kujiendelea kijamii, kujiendelea kiuchumi hadi leo mmefika katika hali ambayo nimewakuta.

Rais Samia: Kubwa zaidi ni kwamba mmesaidia EOTF utekeleza sera ya Maendeleo ya Jamii, sera yetu ya June 1989. Nimetiwa moyo na kazi za wanawake zinavyofanyika kupitia miradi mbalimbali.

Mwisho, Rais Samia awahimiza Watanzania kujitokeza wakati wa zoezi la Sensa na kawatahadharisha kuhusu Uviko-19 na kuhimiza suala la chanjo.
 
Posho
Posho
Posho
[emoji23][emoji1787]
Nchi yangu Tanzania ujanja ujanja mwingi ila anyway zikikufikia hata wewe unapiga kimya ila Kama hauusiki roho inauma kinyama
 
"Maendeleo ya kweli Tanzania ni maendeleo ya watu kiuchumi, kukuza uwezo wa kimapato, kupata huduma za kijamii kama afya, elimu,maji safi na salama pamoja na umeme." Mhe. Samia Suluhu Hassan

#AlipoMamaVijanaTupo
#2022JiandaeKuhesabiwa
#ShirikiUchaguziKwaUadilifu
#KaziIendelee
#MAONESHOYAMIAKA25
#MFUKOWAFURSASAWAKWAWOTE [emoji625]DAR ES SALAAM https://t.co/qLUHvqscia
IMG-20220627-WA0162.jpg
 
Back
Top Bottom