Ushauri wangu kwako ni huu; badala ya kumuita mwenzako mpotoshaji ungeomba mjadala.
Ninachokuhakikishia, hakuna wakati wowote ule ambapo Tabora na Kilimanjaro viliwahi kufikiriwa kuwa jina lanchi kabla ya Tanganyika.
Kabla ya Tanganyika Tabora ilikua bado haijawa named kama mji, ilikua bado ikiitwa Matoborwa na mji uliokuwepo ukijulikana na maarufu ni Kazeh hill. Tabora ilikuja baadaye, wakati tayari kukiwa na miji maarufu kama vile Urambo.
Kilimanjaro uliitwa hivyo huo mlima lakini na wenyewe ulikua hauleweke sana asili yake. Kwani hilo Jina la Kilimanjaro Wakamba wa Kenya ndiyo waliupa hilo jina.
Unasema majina yaliyopendekezwa Wajerumani ni;
1. Smutsland
2.
3. New Maryland
4. Windsorland
5. Victoria
Yaani Mjerumani apendekeze koloni lake liitwe majina ya kiingereza? Hivi hii inaingia akilini mwako kweli?
Una tatizo la ujinga uliokithiri, nakuuliza machache haya ili ujimulike kichwani kama uko sawa
1. Africa kusini wenyeji ndio walipendekeza? Johanesberg ndio walipendekeza wenyeji?
2. Guinea Bissau wenyeji ndio walipendekeza jina hilo?
3. Rhodesia wenyeji ndio walipendekeza jina hilo?
4. Salisbury, Malawi wenyeji ndio walipendekeza jina hilo?
5. Ziwa Victoria ndio walipendekeza wenyeji jina hilo badala ya Nyanza?
6. Bandar Al Salama ( Dar Es Salaam) wenyeji ndio walipendekeza jina hilo badala ya Mzizima?
7. Mikocheni (Michael Chain) wenyeji ndio walipendekza jina hilo?
8. Kawe (Cow Way) wenyeji ndio walipendekeza jina hilo?
9. Lindi (Linda, Lindsay, Belinda) jina hilo lilipendekezwa na wenyeji kama sio wajerumani na waingereza kwa kuwa kulikuwa na wasichana warembo wa kijerumani, kiingereza na kihispania walikuwa wakiishi hapo?
10. Sierra Leone, Cote D'Ivoire, Benin, Niger, Gabon, Cameroon, Senegal, Equatorial Guinea nk je hayo majina ya nchi wenyeji ndio waliyapendekeza?
Fanya utafiti uje na ukweli pingamizi badala ya kubwabwaja bila mantiki