Rais Samia ashiriki sherehe za Jubilee ya miaka 25 ya Mhashamu Askofu Niwemugizi, aombwa kusamehe kodi hospitali za kanisa toka mwaka 2015

Huyu mama anadanganywa sana. zaidi ya iwki hujakaa ofisini, unarudi tu unapaa kwenda sehemu nyingine....urais wa tz unaonekana rahisi sana. kazi yake ni kuhutubu mikutano na kapisha tu
Hili nimelishtukia hata mimi
 
Kwanini huyu mama maadui wa JPM ndio marafiki zake anataka kutuma message gani. Angalia Mange Kimambi, Lissu, Zuhura Yunus nk.
Sio lazima afanane na aliyekuwa bosi wake kama vile mapacha. Wewe unayo taste ya kwako peke yako ya muziki na mimi nina ya kwangu. Wewe unayo aina ya magari unayopenda na mimi ninayo ya kwangu.
 
PASCAL MAYALA wiki hii ulinufurahisha sana uliponiambia kuwa ulisoma na MAREHEMU Mwele Malecela pale Tambaza ,nikakuona kuwa ilikuwa kichwa,Sasa leo Tena unaanza kunichefua Tena niliamini WEWE ni mwandishi uliobobea,uñaanzisha Tena HABARI za kama katuni za TINTIN hadithi za kusadikika kwenye ishu nzito alizozungumza Askofu kwa taifa letu WEWE unaanza soga za HUYU ni msoga gang ,ooh HUYU alikuwa sukuma gang hizo hadithi wenzako tulizifanya kipindi Malecela anataka kupigiwa Kura za maoni kugombea urais tulipiga fitna mpaka ilimfikia MAREHEMU Jk Nyerere,

Kisa watoto wa Malecela kina MAREHEMU Hip walikuwa wanatutesa sana wakija kwenye madisco ya vijana Wa upanga east upanga west na oysterbay yaliyokuwa yanapigwa salenderbridge seaview rungwe Ymca mbowe silver sands msasani kumbe wenzetu kina hip walikuwa wamwibia Mzee wao Hela ya mauzo ya maxi ambayo Malecela alikuwa kiongozi wa kwanza kufuga mgombea oysterbay,leo naona mnaanza style zilezile ambazo mlighalimu hata Kikwete akakosa support ya vijxana kama nyie,Mayalla changanueni mazuri yanasongesha taifa letu
 
Umemuelezea vizuri
 
Mkuu Alex Fredrick, kwanza asante sana kwa kisa hiki cha Padri Kalugendo, kiukweli kisa cha yeye kuvuliwa upadri kinatisha na kusikitisha. Kwa kawaida maungamo hayaruhusiwi, kutumiwa kumuadhibu yoyote hata ukiungama kuua. Padri alivuliwa upadri kwa kufundisha vijana mambo yanayokwenda kinyume cha imani ya Ukatoliki.

Kwa jinsi nilivyokisikia kisa chenyewe, kiukweli kabisa Padri Kalugendo alionewa tuu!.
P
 
Kabisa hairuhusiwi...Marehemu Padre Privatus Karugendo alikuwa mkweli pasi na unafiki ndio kusimamia ukweli wake hatimaye alipoteza U Padre rasmi na kuanza kuishi maisha ya kubangaiza


Jambo lingine ambalo lilikuwa mwiba ni kuwa alikuwa mtetezi wa matumizi ya Condom kinyume na Imani yake hasa Kanisa lake Mama. Siku nilimuuliza kwamba Biblia inakataza na ni Dhambi.. Akajibu hivi:

Ni kweli ni dhambi na pia Hairuhusu lakini akaniambia sisi viongozi wa Dini tunatangaza Altareni au Madhabahuni kwamba dhambi lakini ikifika Usiku tuvaa condom (Unafiki)


Hilo nalo likawa mwiba na zaidi kuambiwa huyu Karugendo ni " Kichaa'.


Karugendo toka miaka 1999 mpaka kufariki mwaka jana aliniambia hawajawi hata siku moja kukutana na Askofu Niwemugizi na akasema kama ingetokea kukutana nae sijui ingekuwaje


Karugendo aliwai kushangaa kuona Askofu Niwemugizi akihoji masuala ya haki na usawa huku yeye Askofu Niwemugizi hajawai hata siku moja kumpa nafasi Padre Karugendo muda wa kuongea au kumsikiliza tu kupitia taratibu za Kanisa zaidi walimtupa na kwenda kupata hifadhi kwa rafiki yake Askofu Benson Bagonza wa KKKT Karagwe
 
Ni kweli ni dhambi na pia Hairuhusu lakini akaniambia sisi viongozi wa Dini tunatangaza Altareni au Madhabahuni kwamba dhambi lakini ikifika Usiku tuvaa condom (Unafiki)
Na wasio vaa, wanatengeneza watoto, ama na wake za watu ama na mabinti za watu, kwa wake za watu, waume zao wanabeba mizigo, lakini kwa mabinti, kwanza familia inapoozwa kwa fungu nene ili kuwafunga mdomo, kisha binti anahamishwa, anawekwa safe place, akiisha jifungua anaendelezwa. Huyo Padri anahamishwa, ziko jela za kiaina. Ila familia inatunzwa!.

Nikiwa DTV nilifanya documentary ya siku ya Ukimwi Duniani. Kanisa Katoliki linahudumia wenye ukimwi kupitia shirika lake la Pasada. Nikafanya mahojiano na Askofu Msaidizi Jimbo Kuu la DSM enzi hizo ni Methodius Kilaini, nikamuuliza
Swali la 1. Kanisa Katoliki linakataza Sex before marriage, na linakaza matumizi ya condom, lakini ukweli unajulikana vijana wa kisasa wanafanya sex kabla ya ndoa, hivyo kusababisha mimba, magonjwa ya zinaa na hata ukimwi, badala ya Kanisa kutumia gharama kubwa kuhudumia wenye ukimwi kupitia Pasada, kwanini wasitoe elimu ya kinga ikiwemo matumizi ya condom ili kuzuia vijana wasiangamie?.
Jibu: "Sex before marriage ni dhambi, elimu ya kinga ni sex abstinence, hakuna kufanya sex kabla ya ndoa. Kuruhusu condom ni kuruhusu zinaa, kamwe hatutaruhusu".
Swali la Pili: Ikitokea mmoja wa wanandoa ameathirika na ukimwi, ili ndoa hiyo iendelee na kumkinga mwanandoa mwingine asiambukizwe, lazima watumie kinga, jee hata kwenye situation kama hii bado condom hairuhusiwi?.
Jibu: " Hairuhusiwi!. Ikitokea mmoja wa wanandoa Wakatoliki ameathirika na ukimwi, huo ndio mwisho wa tendo la ndoa kwa familia hiyo, wanandoa hao wanatakiwa kuishi kama matawoshi, bila tendo la ndoa maisha yao yote yaliyobakia hapa Duniani!. Mwanandoa muathirika aadhibiwe kwa uzinzi wake, na mwanandoa mzima aubebe msalaba wa dhambi ya mwenzake".

Huu ni uthibitisho vitu vingine vya ukatoliki sio reality, Mapadri wana viapo vya useja lakini wanamega kama kawa!. Sijui kuhusu masister kama wanamegwa!. Wanamdanganya Mungu, siku ya mwisho watafanywa kuni!.
P
 
Kwahiyo mumeo akiwa Na ugomvi Na jirani yake Basi Na ww mke wake uingie kwenye ugomvi hata kama haukuhusu?
Katika kuonyesha umoja na ile mantiki ya mwili mmoja inatakiwa akuunge mkono.

Otherwise NOTHING.
 
Ndugu yangu Pascal Mayalla nimesoma replies zako mbili hapo juu bado sijakuelewa unasimamia wapi kulingana na matukio mawili, moja ji hurka na misimamo ya Niwemugizi na pili ni ussue ya msimamo wa matumizi ya kondomu.
 
Wewe jamaa nina wasiwasi na wewe,nimefanya kazi Jimbo Katoliki la Rulenge -Ngara,kwa miaka karibia sita hivi,huyo Fr.Karugendo,jina lake la kwanza umedanganya haitwi Bernard Bali ni Privatus.Halafu Sababu unazozisema sio Sahihi,tafuta Canon Law usome Sababu zinazoweza kumfanya Padre akose/afukuzwe Upadre,na taratibu za mtu kufukuzwa Upadre,kimsingi ni mlolongo mrefu,sio km ulivyoeleza kwa Sababu nyepesi hizo.
 
Umemwelewa Baba Askofu lkn au umekommenti tu ili mradi??.
 
Mzee, Ukitaka kuwa Hakimu mzuri Jifunze kusikiliza na upande wa pili.Ukisikiliza upande mmoja tu na kuondoka na maoni unakuwa hujatenda haki,kwa hiyo ungemuuliza Askofu Severini Niwemugizi naye akupe sababu wenda ungepata kitu tofauti.
 
Huyo askofu ni mpuuzi, angetoa angalau mfano mmoja tu unaoonyesha utukwazaji wa Mh Samia katika level ya Mwenyezi Mungu. Kwanza angejiangalia yeye mwenyewe anavyonyenyekewa na wafuasi wake, pumbavu kabisa
 

Hata Yesu alipokuja, hakuja kwaajili ya watu wema, alikaa na makahaba na watoza ushuru, ili wapate kutubu. Sioni logic ya kuwatenga hao watesa watu unadhani wataujuaje ukweli na kuokoka? Hapo ndipo mnapokosea
 
Huyu mama anadanganywa sana. zaidi ya iwki hujakaa ofisini, unarudi tu unapaa kwenda sehemu nyingine....urais wa tz unaonekana rahisi sana. kazi yake ni kuhutubu mikutano na kapisha tu
Anasumbuka tu..ngoja aanze kuletewa mawaraka ya pasaka..ni jambo la muda tu....na kwanini kila siku ni kanda ya ziwa tu? nafikiri ziara ya saba hii kama sio nane aje na kusini basi
 
Anasumbuka tu..ngoja aanze kuletewa mawaraka ya pasaka..ni jambo la muda tu....na kwanini kila siku ni kanda ya ziwa tu? nafikiri ziara ya saba hii kama sio nane aje na kusini basi
yaani ni aibu urais kwake ni kanda ya ziwa kufurahisha wasukuma, kanda ya kaskazini akidhani anaivuruga chadema na kwao zanzibar
 
Hata Yesu alipokuja, hakuja kwaajili ya watu wema, alikaa na makahaba na watoza ushuru, ili wapate kutubu. Sioni logic ya kuwatenga hao watesa watu unadhani wataujuaje ukweli na kuokoka? Hapo ndipo mnapokosea
Kwahiyo hawa watesi wetu wakihudhuria ibada hizi za kualikwa unaona watarudi kwenye mstari? Hujui kama wanafanya siasa tu?

Angalau Yesu alikuwa na ubavu wa kuwaambia wanaokosea bila kumung'unya maneno.
 
Kwanini huyu mama maadui wa JPM ndio marafiki zake anataka kutuma message gani. Angalia Mange Kimambi, Lissu, Zuhura Yunus nk.
Kwa hiyo ulitaka arithi maadui wa magufuli unajitambua kweli wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…