Rais Samia ashiriki uzinduzi wa Album ya Harmonize Ukumbi wa Mlimani City, leo Mei 25, 2024

Rais Samia ashiriki uzinduzi wa Album ya Harmonize Ukumbi wa Mlimani City, leo Mei 25, 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki uzinduzi wa album ya Harmonize leo tarehe 25 Mei, 2024 katika ukumbi wa Mlimani City.


View: https://www.youtube.com/live/PafgRqkHmNo?si=oHJtx2WgTWFmEp9k

RAIS SAMIA
Amemshukuru Msanii Harmonize kwa kumualika kwenye hafla hii aliyoiita 'Usiku wa kuutukuza muziki wa Mama'

Rais Samia ameoneshwa kufurahishwa na ukuaji wa Harmonize kwani alivyo sasa ni tofauti na alivyokuwa miaka 8 nyuma.

Amesema mapito ya kimahusiano aliyopitia Harmonize huwapata vijana wengi, na ametaja baadhi kama Ray Vanny, Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz.

Amewapongeza wanawake wote waliolea na kukuza watoto hadi kuwafikisha kwenye mafanikio, wanawake na jeshi makini na jeshi imara.

Amesema amekuwa na kawaida ya kubeba wafanyabiashara kwenye ziara zake, sasa ataanza kwenda na wasanii ili kufungua zaidi nchi na kukuza tasnia hiyo.

Amewasaa wasanii wa muziki na filamu kuwekeza kwenye maisha yao kwani hawatafanya kazi hizo milele. Uwekezaji huo utawasaidia pindi watakapokuwa hawawezi tena kufanya kazi wanazofanya sasa.

Mh. Rais Dkt Samia awakumbuke pia wasomi wa jalalani toka UDSM kwenye misafara yake. Maana wana njaa kweli kweli angalau watoke nao.
 
Huu nao ni ujinga kumtukana mtu ambaye anaweza kuwa mama yako kabisa na akawazaa nyinyi kama kumi! Huu ni ujinga! Kuna ubaya gani Rais kwenda kumuunga mkono msanii wake? Kwani sanaa si inatoa ajira jamani? Mbona mnapinga kila jambo?
Ndio hapo Sasa nashangaa MTU ana stress zake from know where anajikuta ana tukana ovyo ovyo watu wa umri wa mama yake
 
Back
Top Bottom