Rais Samia ashuhudia utiaji wa saini wa hati ya ushirikiano nchini Uganda

Rais Samia ashuhudia utiaji wa saini wa hati ya ushirikiano nchini Uganda

tamsana

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2012
Posts
3,739
Reaction score
8,044
Tujisomee.
Aliyepata kapata!

IMG-20220510-WA0016.jpg
 
Naona hapo tutanunua ARVs toka Uganda, na pia tumewakubalia kupunguza bei ya usafiri kwa lori moja kwa dola 10 za kimarekani.

Wao watatuletea tani elfu 10 za sukari, kwani hiyo sukari watatuletea bure?

Sijaona sisi tulichopata toka kwa hayo mazungumzo, naona waganda wanatupiga sana.
 
Kwa hiyo Uganda wanaweza kutengeneza dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ila sisi hatuwezi.?

Kingine tujiulize kwanini Uganda ana ziada ya sukari kuuza nje ya nchi sisi tunashindwa nini?

R.I.P Magufuli sijui Azam ameishia wapa na mpango wake wa kuzalisha sukari nchini.

Mwisho naona mhitasari wa mazungumzo faida ni kwa Uganda tu, Sijaona Tanzania itakavyofaidika.
 
Utapata vidonda vya tumbo!!..wewe ni mtanzania kweli!!?..huna jema!!...utasema ulikuwepo kwenye makubaliano
 
Mbona kwa miaka mingi sana Tz tulikuwa tunazalisha ARVs?
Bado ninakumbuka sana lile skendo la bench fulani za ARVs feki la kile kiwanda cha Ramadhani Madavida na Mkewe (makada wa CCM) hapa Dar.

Tuliacha lini kuzalisha ARVs?
Kwanini tuliacha kuzalisha?
Kwanini tununue na tusizalishe wenyewe?
Kabla ya mkataba huu na Uganda, tulikuwa tunapata wapi ARVs?
 
Naona ni katika jitihada za kupunguza gharama za maisha kwa watanzania, huenda na bei ya sukari itapungua [emoji848]
Kama ana mipango mizuri aachane na masuala ya kuagiza vitu Kama sukari. Wezesha viwanda vya hapa, bakhresa kafungua kiwanda bagamoyo. Serikali inapaswa kumpa support 100% ili azalishe zaidi na zaidi na sisi tuuze huko nje
 
Kwa hiyo Uganda wanaweza kutengeneza dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ila sisi hatuwezi.?

Kingine tujiulize kwanini Uganda ana ziada ya sukari kuuza nje ya nchi sisi tunashindwa nini?

R.I.P Magufuli sijui Azam ameishia wapa na mpango wake wa kuzalisha sukari nchini.

Mwisho naona mhitasari wa mazungumzo faida ni kwa Uganda tu, Sijaona Tanzania itakavyofaidika.
POPULATION.
 
Mbona kwa miaka mingi sana Tz tulikuwa tunazalisha ARVs?
Bado ninakumbuka sana lile skendo la bench fulani za ARVs feki la kile kiwanda cha Ramadhani Madavida na Mkewe (makada wa CCM) hapa Dar.

Tuliacha lini kuzalisha ARVs?
Kwanini tuliacha kuzalisha?
Kwanini tununue na tusizalishe wenyewe?
Kabla ya mkataba huu na Uganda, tulikuwa tunapata wapi ARVs?
Ni aibu kwenda kununua Uganda ikiwa uwezo wa kuzalisha tunao.
Hata sukari uwezo wa kuzalisha tunao
Kuna vitu vya kuagiza nje Ila sio kwa vitu Kama hivyo.
Kuna siku hata unga wa ugali tutaagiza nje
 
Naona hata taarifa ya Ikulu imekaa kimchongo mchongo sana.
Kwa mfano inasema tozo za usafirisha mizigo ya Uganda itapunguzwa mpaka kuwa dola 10, lakini haisemi hapo awali tozo ilikuwa ni kiasi gani?

Kitaaluma unapotoa ripoti ya ulinganifu (comparative analysis) ni lazima utamke pande zote mbili za figure/facts zinazozungumziwa ili kuwa proper reference analysis, unapotaja upande mmoja tu, unakuwa umesema nusu ya ukweli na kuficha nusu nyingine ya ukweli.
 
Back
Top Bottom