Kitu pekee nachoweza amini kama sababu ya Asha Rose Migiro kuondolewa U.K. itakuwa kaomba mwenyewe umri umeenda anataka arudishwe kupumzika.
Aisee yule mama uwezi kuamini kama alishakuwa makamu wa UN na kashika nafasi kubwa Tanzania, hana tofauti na mama ya nyumba ya jirani mitaa yetu ya uswazi alieridhika na maisha na kila mtoto mtaani anamuona wake.
Ukikutana na Migiro ni very humble, ukiona mtu ana tatizo na yule mama una kila sababu ya kuamini tatizo ni huyo mtu mwingine. Unapata picha kwanini huko serikalini kadumu kwa muda mrefu aisee yule mama mstaarabu sana na accessible kwa mtu yeyote.