Rais Samia: Asiyejua anasema Serikali inakopa tu, kwani tunakopa kununua sare za harusi?

Rais Samia: Asiyejua anasema Serikali inakopa tu, kwani tunakopa kununua sare za harusi?

Rais Samia amedai Wafanyabiashara wadogo na wakati wengi wao wanakimbia ulipaji kodi hali inayosababisha kuingia kwenye mikopo na "Asiyejua anasema Serikali inakopa tu, kwani tunakopa kununua sare za harusi?"

Soma, Pia: Luhaga Mpina: Taifa limebakiza 4.6% tu kufikia Ukomo elekezi wa Deni la nje. Kauli ya 'Deni letu ni himilivu' karibu inapotea

Ilikuwaje tukashindwa "kukopa" ili kuboresha zaidi Bandari mpaka "tukaibinafsisha" ??

"Sitegemei Baada ya maboresho tuliyofanya hapa Bandari ya DSM tutakuja kumpa mwekezaji, maana imekuwa ni Kawaida yetu Baada tu ya kufanya maboresho tunakimbilia kutafuta mwekezaji" Magufuli
 
Tunampa, wawekezaji binafsi Wana uzoefu na kazi hizo za biashara.

Njia mojawapo ya kuwavutia ni kuwajengea miundombinu basic sio wao waje wawajenges harafu mkishindwana muwatomue.

Jenga wewe harafu muite mkishindwana mtimue atakuachia Bandari Yako.
 
Mtaani kuna mikopo mpaka imepewa majina ya nyonya damu. Mheshimiwa amenikumbusha kuna ndugu yangu huwa anawakopesha wakulima pesa kwa ajili ya kulipwa mahindi. Kwetu mahindi yanavunwa kuanzia mwezi Mei, lakini cha kushangaza hadi huo mwezi wa mavuno kuna wakulima huwa wanaenda kukopa kwa huyo ndugu yangu gunia wanakopa Sh 20k wakati angevumia mwezi mmoja tu hilo gunia angeuza 45k. Huwa nabaki kuwaonea tu huruma hao wakulima.
 
Kwa kifupi nachoona serikali ya sasa imeshindwa kusimamia watanzania kulipa kodi, tumeshindwa kuzitumia fursa na malighafi tulizonazo kuzalisha na kutengeneza pesa na kufanya uchumi ukuwe. Mimi mwenyewe nafanya biashara lakini uwezi tegemea mikopo kukuendeshea biashara yako. Labda tu niseme kwa kifupi mimi mwenyewe sielewi taifa letu tunaelekea wapi yani ni bora liende. Kwa mimi binafsi naona tuwe na sera kama taifa na sio kama chama yani wewe chama njo na mikakati yako utawezaje kutekeleza sera ya taifa basi.
 
Back
Top Bottom