Rais Samia ataka kikosi kazi cha nishati safi ya kupikia

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1667329736305.png

Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuanzishwa kwa kikosi kazi kitakachoshughulikia nishati safi ya kupikia, lengo likiwa kuanzisha safari ya kulitoa Taifa kwenye matumizi ya nishati isiyofaa. Kikosi kazi hicho ambacho hakitakuwa cha Serikali pekee, kitahusisha pia sekta binafsi na wadau wa maendeleo kitakuwa na kazi ya kuchambua sera za Serikali na mapendekezo ya wadau.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndiye atakayeongoza kikosi kazi hicho kwa ngazi ya mawaziri ambapo uratibu utafanyika chini ya Wizara ya Nishati. Rais Samia ametoa maelekeo hayo leo Novemba Mosi wakati wa kongamano la kitaifa la nishati safi ya kupikia linalofanyika leo na kesho jijini Dar es Salaam.

Amesema kikosi kazi hicho kitakuja na mpango mkakati ambao utaiongoza Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kutafuta suluhu ya nishati safi na endelevu ya kupikia. Takwimu zinaonyesha kuwa kaya zinazopikia kwa kutumia mitungi ya gesi ni asilimia 5, umeme asilimia 3 na nishati nyingine safi asilimia 2.2.

“Hii inaonyesha bado kuna kazi ya kuhamasisha matumizi ya nishati iliyo safi na salama. Tunapaswa kuwa na mkakati madhubuti wa kisera na kibajeti pamoja na kuweka mazingira wezeshi katika kutatua changamoto za upatikanaji wa nishati safi.

“Kwenye hili Serikali peke yetu hatuwezi tunapaswa kwenda sambamba na sekta binafsi, nashukuru baadhi yao wameanza kujitokeza tunakwenda nao sambamba lakini si kisera kwa sababu ni fursa ya biashara hivyo kuna haja ya kuwa na sera inayoshughulikia suala hili,” amesema Rais Samia.

MWANANCHI
 
Mwamba amejikausha kama hayupo nakumbuka enzi za kupiga nyungu
Screenshot_20221101-221156.png
 
Turudi kwenye mada sasa. Gesi za kupimiana kwenye mitungi sio saizi yetu hasa ukizingatia Ntwara hapo enzi za mkwere gesi iliwekwa ktk matumizi(sina uhakika kama inafaa kwa matumizi ya majumbani)

Serikali ipiganie tuwe na umeme wa kutosha na kisha tuwe kama nchi zilizo endelea majiko yawe ya gesi ya kufungiwa hafi nyumbani na majiko ya umeme tu
 
Wanagangaika na mitungi wakati walitwambia Hesj ya Mtwara itasambazwa hadi kwenye majumba😅😅
 
Hii yote ni ili tu.....
Rostam Aziz

Apate tenda ya kusambaza "Taifa Gas"
Nchi nzima?

Ina maana kwamba Rostam alikwisha jipanga kitambo kwa hii project.
Ndio sababu ya kuitwa "Taifa Gas"!

Na ndio sababu rasmi ya Makamba kuizungusha nchi nzima akijifanya kuwahirumia kina mama dhidi ya moshi wa kuni huko vijijini.

Je!
Kikosi kazi cha nini,wakati inajulikana kwamba "STAMICO" tayari walikwisha zindua mradi kabambe wa nishati mbadala ya kupikia.

Mkaa wa mawe,ulikwishaanza kuchakatwa na STAMICO na kufaa kutumika kwa kupikia.

Na waziri wa madini Biteko akauzindua Rasmi.
Na taifa likatangaziwa rasmi.

Pia Rais Samia akahudhuria hadi kwenye Banda la maonyesho ya huo mkaa!

Ukiwa umekwisha kuwa packed kwenye mifuko kuanzia kilo 10 na kuendelea.

Halafu mnaharibu pesa za walipa kodi kwa Makongamano yasiyo na tija kwa wananchi,zaidi ya hso hao Cartel's kuendelea kujipanga ili kuifilisi nchi hii.

Ifike mahali tuseme hapana!

View attachment 2404516View attachment 2404517
 
Hii inchi ndo maana atuendelei sasa kikosi kazi cha kazi kani kubwa kuzidi kutimiza malengo ya kusambaza gesi Mtwara majumbani..
 
Rostam The Master mind...kawakalisha wote hao wadiscuss nishati mbadala...
 
Hii yote ni ili tu.....
Rostam Aziz

Apate tenda ya kusambaza "Taifa Gas"
Nchi nzima?

Ina maana kwamba Rostam alikwisha jipanga kitambo kwa hii project.
Ndio sababu ya kuitwa "Taifa Gas"!

Na ndio sababu rasmi ya Makamba kuizungusha nchi nzima akijifanya kuwahirumia kina mama dhidi ya moshi wa kuni huko vijijini.

Je!
Kikosi kazi cha nini,wakati inajulikana kwamba "STAMICO" tayari walikwisha zindua mradi kabambe wa nishati mbadala ya kupikia.

Mkaa wa mawe,ulikwishaanza kuchakatwa na STAMICO na kufaa kutumika kwa kupikia.

Na waziri wa madini Biteko akauzindua Rasmi.
Na taifa likatangaziwa rasmi.

Pia Rais Samia akahudhuria hadi kwenye Banda la maonyesho ya huo mkaa!

Ukiwa umekwisha kuwa packed kwenye mifuko kuanzia kilo 10 na kuendelea.

Halafu mnaharibu pesa za walipa kodi kwa Makongamano yasiyo na tija kwa wananchi,zaidi ya hso hao Cartel's kuendelea kujipanga ili kuifilisi nchi hii.

Ifike mahali tuseme hapana!

View attachment 2404516View attachment 2404517
Huu ulitakiwa uwe uzi mpya kabisa, tunachezewa na kudanganywa!
 
View attachment 2404451
Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuanzishwa kwa kikosi kazi kitakachoshughulikia nishati safi ya kupikia, lengo likiwa kuanzisha safari ya kulitoa Taifa kwenye matumizi ya nishati isiyofaa. Kikosi kazi hicho ambacho hakitakuwa cha Serikali pekee, kitahusisha pia sekta binafsi na wadau wa maendeleo kitakuwa na kazi ya kuchambua sera za Serikali na mapendekezo ya wadau.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndiye atakayeongoza kikosi kazi hicho kwa ngazi ya mawaziri ambapo uratibu utafanyika chini ya Wizara ya Nishati. Rais Samia ametoa maelekeo hayo leo Novemba Mosi wakati wa kongamano la kitaifa la nishati safi ya kupikia linalofanyika leo na kesho jijini Dar es Salaam.

Amesema kikosi kazi hicho kitakuja na mpango mkakati ambao utaiongoza Serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kutafuta suluhu ya nishati safi na endelevu ya kupikia. Takwimu zinaonyesha kuwa kaya zinazopikia kwa kutumia mitungi ya gesi ni asilimia 5, umeme asilimia 3 na nishati nyingine safi asilimia 2.2.

“Hii inaonyesha bado kuna kazi ya kuhamasisha matumizi ya nishati iliyo safi na salama. Tunapaswa kuwa na mkakati madhubuti wa kisera na kibajeti pamoja na kuweka mazingira wezeshi katika kutatua changamoto za upatikanaji wa nishati safi.

“Kwenye hili Serikali peke yetu hatuwezi tunapaswa kwenda sambamba na sekta binafsi, nashukuru baadhi yao wameanza kujitokeza tunakwenda nao sambamba lakini si kisera kwa sababu ni fursa ya biashara hivyo kuna haja ya kuwa na sera inayoshughulikia suala hili,” amesema Rais Samia.

MWANANCHI

Anahangaika tu ili wapate pesa ya kampeni.. kama anataka watu waache kuni apunguze bei ya gesi na umeme.

Kwisha.

Tukidhaweza kupika makande kwenye gesi hapo biashara imeisha
 
Back
Top Bottom