Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kama Samia, ushahidi wenyewe aliokuwa anasema anao, ndiyo huu, basi kafeli sana. Na hao waliotengeneza hizi chats, kwa vyovyote wanamdharau sana Rais, ina maana wanamwona hamnazo, hivyo ataamini tu!! Si ajabu watakuwa wamemdanganya kuwa hao vijana na hizo silaha ziliandaliwa na marehemu Ally, ndiyo maana jana, Rais Samia ametumia muda mwingi kukejeli kifo cha Ally.Kiukweli katika siku mojawapo ambayo nilijisikia mnyonge ni jana aiseee nilijihisi nimepigwa shot ya umeme baada ya kukaa chini na kusikiliza hotuba ya Rais Samia kiukweli Rais samia anapotoshwa na wala haambiwi ukweli sijui kwanini sijui wasaidizi wake wanataka afeli au sijui nini kinamsibu huyu mama wa watu
Yaani anaamini kuna chama cha upinzani kinataka kufanya foju kweli? Yaani mheshimiwa mbowe awaorganize wenzake kufanya uharibifu kweli? Mheshimiwa mbowe huyu huyu ninae mjua Mimi ambaye olmost zaidi ya miaka 30 yupo kwenye siasa za nchi hii huyu mzee ana hekima sana na wala hana nongwa na mtu afanye uharibifu kweli? Aisee
Mheshimiwa Rais hii screenshot na wewe unaamini? Kwamba eti bonifasi Jacob anaorganize wahuni wa mtaa eti wakaripue vituo vya polisi? Bonifasi jacob huyu huyu alumni wa UDsm kiukweli nimechoka na kufadhaika sana
Na ninyi wasaidizi wa Rais mpo tayari Rais anapotea?na kupotoshwa? Kwa ajili ya maislahi yenu tu hamjui kwamba ipo siku mungu atawalipa kwa ouvu wenu? Rais samia kuwa makini unapotoshwa sana na utakuja kujua baadae sana ya kwamba unapotoshwa wakati upo nje ya madaraka kama mwenzio mkapa kama usiposhituka sasa.
NB
Moderator acheni uchawa acheni huu Uzi
Mungu wa mbinguni, tunaomba laana juu ya watu hawa maana kisasi ni chako Mungu wa milele.