Rais Samia atangaza siku 5 za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth aliyekuwa Mkuu wa Nchi ya Tanganyika

Rais Samia atangaza siku 5 za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth aliyekuwa Mkuu wa Nchi ya Tanganyika

Huyu atakuja kufanya hii nchi mwanamke asije tena kuongoza maisha yote.
Yani hata jiwe angekuwa ndo Rais wa hii nchi, bendera ingepepea nusu mlingoti tu, malkia ni mkuu wa nchi za JUMUIYA ya MADOLA, Tanzania ni moja wapo. Na malkia aliipatia uhuru Tanganyika
 
Tunapumzika siku ngapi ukiachana na bendera kuwa nusu mlingoti
 
Kazi kama kawa sema ni bendera tu ndiyo zitakua nusu mlingoti!!

Sasa Kama Ni Bendera Tuu Ina Maana Gani?
Kama Hatupumziki?
Kwani Bendera Ikipepea Nusu Mlingoti mimi au wewe Unakosa Kula?
Kupumzika? Si Inakuwa kama Jana ,Juzi Siki iliopita,
 
Kama kawaida, wa mihemko wamekuja juu, wameshapata mwanya wa kuendeleza mashambulizi yao yenye hoja mufilisi.
 
Hakuna ata siku moja ya mapumziko, kweli? mama usitufanyie hivyo wanao

Nakuunga Mkono Mkuu!
Mapumziko ni Muhimu,Wengine wataingiza Kodi ya Mapato Kwa Kufanya Kazi Overtime na Hivyo Kuliingizia Taifa Fedha…
Hivyo Iwe Mapumziko tuu kaka ili Watu waingize Kodi na Sisi Tupumzike Kaka tuwe karibu na familia[emoji1787][emoji2957][emoji736]
 
Mimi kama Hatupunziki sioni tofauti!
Labda wewe uniambie Bendera ikipepea Nusu Unakosa nini?
Mi Nataka Tupumzike wewe unaongelea Nadharia sijui utumwa sijui nini…
Mama leta mapumziko hapa Ili iwe na Impacts.
Hivi mimi hapa Washushe bendera au wasichushe naamka tuu naenda Kazini tofauti Iko wapi??? Bora tupumzike Tujue Kuna Impactss
 
Rais Samia atangaza siku tano za maombolezo kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II kilichotokea tarehe 8 Septemba, 2022.

Maombolezo hayo yataanza tarehe 10 Septemba hadi tarehe 14 Septemba.

Katika kipindi hicho bendera za Tanzania zitapepea nusu mlingoti, ikiwa ni pamoja na kwenye balozi zetu.

Taarifa kamili[emoji116]View attachment 2351886
Asitusumbue na yeye
 
Watu kulalamika Kwa vitu visivyo na maana Sasa hayo maombolezo yanakuathili Nini?Kazini unakwenda,tozo zipo,kama mbususu unachakata,bill unalipa nk

Mkuu nimekupa Like….Nqomba Kila Anaelalamika muwekee hii comment yako,
Nami Nawashangaa majitu eti yanalalamika hao ndio wamekaririshwa Siasa/History ya Vitu Visivyokuwa na Mashiko,
Bendera Kushushwa bado Naenda Kazini,Naamka asubuhi,Nakula,Nalipa Kodi,Yaani Bendera Ishushwe isishushwe wala hata Sijui,Bora tupumzike Tujue Moja,
Ili wengine waiingizie Mapato Serikali Kupitia Overtime As PAYE,Wengine Tukae na Familia na watoto walitumiss,
Serikali inatakiwa Ipate Hela Kupitia Mapumziko kama Haya Kwa Overtime tofauti na Hapo Hakuna Mapato ya Ziada…
Tupumzikeeeee[emoji30]
 
Vijana wa siku hizi bwana. Unalalamika sababu ya kutokujua kwako mambo ya kijiopolitiki. Unasahau huyu amewahi kuwa mkuu wa nchi hii enzi hizo ikiitwa Tanganyika, na pia amekuwa kiongozi wa jumuiya ya madola ambayo Tanzania ni mwanachama. Jifunzeni kutohemuka mnapokutana na jambo. Jipeni muda wa kutafakari kabla ya kubwabwaja. Isitoshe kutangazwa kwa siku hizo za maombolezo kumeathiri vipi maisha yako?
Hawawezi kuyaelewa hayo ndugu yangu maana uwezo wao ni mdogo hawajuwi hata historia ya nchi hii Ndio maana vinywa vyao vimejaa matusi tu, hawana adabu Wala heshima
 
Lazima uelimishwe maana nyie hata hamjuwi historia ya nchi hii Zaid ya matusi tu, hamjuwi nchi hii ilikotoka na mchango wa malkia
Sisi hatumuongelei malkia.....umeona kweny comment yangu nmetaja neno malkia....au hujui kusoma na ww....ww unaejua historia imekupa kula
 
Back
Top Bottom