Pre GE2025 Rais Samia atavunja Rekodi ya Jakaya Kikwete ya 2005 kwa kupata kura nyingi tangia kuanza kwa Mfumo wa vyama vingi

Pre GE2025 Rais Samia atavunja Rekodi ya Jakaya Kikwete ya 2005 kwa kupata kura nyingi tangia kuanza kwa Mfumo wa vyama vingi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuanzia leo naanza kuunga mkono nyuzi zako unazochapisha hapa jamvini, maana nimegundua wewe ni miongoni mwa watu wasiompenda Samia kama mimi.

Na ndiyo maana unampa ushauri potofu na sifa za kijinga ili aendelee kujisahau halafu 2025 adondoke kama embe dodo.

Hongera sana Lucas Mwashambwa kwa akili hii kubwa, nimechelewa sana kung'amua.
 
Lucas yuko kwenye payroll ya bilionea Sugu Moto Chini 🔥
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mpaka sasa Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete Rais Mstaafu wa awamu ya nne anashikilia rekodi ya kupata kura nyingi na kwa asilimia kubwa katika awamu yake ya kwanza tu katika kutafuta nafasi ya kuingia ikulu tangia mfumo wa vyama vingi uanze.

Napenda kuwakumbusheni na kusisitiza kuwa hoja yangu ipo katika uchaguzi wa kwanza wa mgombea husika. Yaani namaanisha kuwa asilimia alizozipata Hayati Benjamini Mkapa mwaka 1995 alipokuwa anagombea Urais kwa Mara ya kwanza na asilimia alizozipata Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Magufuli Mwaka 2015 alipokuwa anagombea Urais kwa Mara ya kwanza .

Hakuna kati yao aliyefanikisha kupata kura na asilimia alizozipata Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete.kwa sababu Hayati Benjamini Mkapa alipata Asilimia 61 na hata Hayati Dkt Magufuli hakufikia kura na asilimia hizo katika awamu yake ya kwanza ya kuomba Urais alipopambana na Hayati Edward lowassa.

Wakati Mheshimiwa Dkt Kikwete yeye alipata kura takribani asilimia 80 ya kura zote. Na huyu ndiye mgombea wa CCM ambaye alikuwa anakubalika sana hapa nchini kuwahi kutokea tangia mfumo wa vyama vingi uanze katika awamu yake ya kwanza ya kuutafuta Urais. Ni mgombea ambaye alikuwa na mvuto mkubwa sana wa kisiasa na alikubalika na watu wa vyama vyote.

Lakini katika awamu yake ya pili yaani 2010 kura zake katika sanduku la kura zilishuka na hata asilimia za kura zake zilishuka ,wakati Hayati Benjamini Mkapa pamoja na Hayati Dkt John Magufuli wao asilimia zao zilipanda sana katika awamu zao za pili katika kutafuta na kutetea nafasi zao. Hapa napo pana mjadala ambao ulipelekea Rais Dkt Jakaya Mrisho kushuka .ambapo siwezi kujadili hapa maana inahitaji andiko la peke yake kuweza kuwachambulia vizuri sana na kwa undani.

Sasa nikiangalia hali ya kisiasa ilivyo hapa Nchini kwa sasa,hasa kukubalika na umaarufu wa Rais Samia kwa watanzania na namna anavyopendwa na kuungwa mkono na watu wa makundi mbalimbali na wa vyama vyote .naona Jemedari wetu Daktari Mama Samia akienda kuivunja Rekodi hiyo inayoshikiliwa na Daktari Jakaya Kikwete kwa kupata kura nyingi za kishindo hapo Mwakani katika Historia ya Taifa letu.

Naona akienda kuvuna mamilioni kwa mamilioni ya kura za ndio katika sanduku la kura na kupata asilimia kubwa zitakazoweka rekodi itakayodumu kwa muda mrefu. Hii ni kwa kuwa ndani ya muda mfupi amefanikiwa sana na kwa kiasi kikubwa sana kugusa Maisha ya mamilioni ya watanzania,kuinua maisha ya watu,kuleta unafuu wa kimaisha ,kujenga matumaini kwa watu,kuwawezesha vijana ambalo ndilo kundi kubwa hapa Nchini. Ambapo sasa vijana wanamkubali sana Rais Samia.lakini kubwa kuliko ni kuwa ameleta maendeleo makubwa sana katika kila secta ambayo siwezi kumaliza kuyaorodhesha hapa jukwaani.View attachment 3080513

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Chawa uma hapo hapo usiachie hadi uteuzi uje bana meno chawa
 
Halafu wanatoka hapo wanampa Dotto magari shavu.

Iła MaCCM yana roho mbaya sana, wawakumbe na vijana wao wa JF pia, hata mwaliko Kizimkazi kimya.

Kijana amempambania sana bi-tozo anahitaji recognition na yeye.
 
Wewe Simbilisi kwani mh Rais Samia anagombea Kwa mara ya kwanza 2025

Nyie mtatawaliwa na Wanyakyusa milele na milele aisee 😂😂😂

Yaani Wasafwa ndio wanakutegemea Wewe na Choicevariable ndio muwaondolee aibu ya kukosa mbunge 😂😂😂😂 Bure Kabisa

Afadhali yule Mnyiha Nyagali 🐼
Kweli wewe ni sifuri kabisa kichwani. Kwani mara ya kwanza Rais Samia aligombea lini Urais na mgombea Mwenza wake alikuwa ni nani? Yaani wewe huwa hujitambui kabisa .unafanyaga kazi ya kukurupuka tu kama kuku anayetaga
 
Kuanzia leo naanza kuunga mkono nyuzi zako unazochapisha hapa jamvini, maana nimegundua wewe ni miongoni mwa watu wasiompenda Samia kama mimi.

Na ndiyo maana unampa ushauri potofu na sifa za kijinga ili aendelee kujisahau halafu 2025 adondoke kama embe dodo.

Hongera sana Lucas Mwashambwa kwa akili hii kubwa, nimechelewa sana kung'amua.
Utaendelea kuumia sana na chuki zako binafsi kwa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi anayeendelea kuchanja mbuga katika mioyo ya mamilioni ya watanzania.
 
Kweli wewe ni sifuri kabisa kichwani. Kwani mara ya kwanza Rais Samia aligombea lini Urais na mgombea Mwenza wake alikuwa ni nani? Yaani wewe huwa hujitambui kabisa .unafanyaga kazi ya kukurupuka tu kama kuku anayetaga
Wewe ni Simbilisi

Mh Rais Dr Samia yuko madarakani Kwa kura zipi?

Wewe ndio Sababu Dr Mwansasu PhD amekushtukia Kwa kuwapaka Viongozi mafuta Kwa mgongo wa chupa

Bado Kafulila na Makonda ndio hawajagundua Michezo Yako 😂😂😂

Unadhani kwanini Moto Chini alikuzuia kuendelea Kutangaza namba Yako ya Simu mitandaoni?😃😃😃😃🔥🔥

Nimemaliza baadae ulale Unono 😂
 
Sio shabiki wa siasa though siasa runs the country ktk mambo karibia yote. Kuhusu siasa za nchi hii its obvious ccm will again take a lead, hata kwa bao la...nikiwaangalia watanzania walivyo na vile wapinzani wa ccm walivyo naona kabisa ccm itatumia techniques zake za mara zote na itaishinda. Watanzania wanapenda kubadili utawala lakin pa kuanzia wanakosa. So ikifika wakati wa uchaguzi wanaona bora ccm iendelee na hata kama hawakuridhika na mchakato wake ila wanasemaga aah patelea mbali haiwahusu.
 
Kweli wewe mzee unazeeka vibaya sana na ukurupukaji? Umeelewa andiko langu? Andiko linasema katika awamu ya kwanza. Nani aliyepata kura 80% katika awamu yake ya kwanza ya kutafuta urais?

Tatizo lako wewe mzee ni mkurupukaji sana na mtu ambaye hujatulia kichwani.wewe ni kuandika tu kila kitu kinachokujia kichwani mwako.
Samia itakuwa awamu ya pili ya utawala wake
 
Wewe ni Simbilisi

Mh Rais Dr Samia yuko madarakani Kwa kura zipi?

Wewe ndio Sababu Dr Mwansasu PhD amekushtukia Kwa kuwapaka Viongozi mafuta Kwa mgongo wa chupa

Bado Kafulila na Makonda ndio hawajagundua Michezo Yako 😂😂😂

Unadhani kwanini Moto Chini alikuzuia kuendelea Kutangaza namba Yako ya Simu mitandaoni?😃😃😃😃🔥🔥

Nimemaliza baadae ulale Unono 😂
Hili jitu huwa nawaambia halina akili japo lipo UWT pale
 
Sio shabiki wa siasa though siasa runs the country ktk mambo karibia yote. Kuhusu siasa za nchi hii its obvious ccm will again take a lead, hata kwa bao la...nikiwaangalia watanzania walivyo na vile wapinzani wa ccm walivyo naona kabisa ccm itatumia techniques zake za mara zote na itaishinda. Watanzania wanapenda kubadili utawala lakin pa kuanzia wanakosa. So ikifika wakati wa uchaguzi wanaona bora ccm iendelee na hata kama hawakuridhika na mchakato wake ila wanasemaga aah patelea mbali haiwahusu.
CCM ndio tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo
 
Back
Top Bottom