Rais Samia atembelea Barabara ya Mzunguko Dodoma na kuzungumza na wananchi Juni 14, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais Samia akitembelea Barabara ya Mzunguko Dodoma (Km. 112.3) na Kuzungumza na Wananchi, leo tarehe 14 Juni, 2025.
====

​

Rais Samia ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3. Akiwa katika hafla hiyo iliyofanyika Mtumba, Dodoma, Rais Samia alizungumza na wananchi na kueleza dhamira ya serikali kuendeleza miradi ya kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa pia na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na mgeni rasmi wa Rais Samia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina. Rais Samia alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na muhimu kwa maendeleo ya Tanzania, hivyo serikali inaendelea kutafuta mkopo nafuu, yaani mkopo usio na riba kubwa ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa kwa wakati.

​

Akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, alisema kuwa barabara hiyo ya mzunguko itapunguza kwa kiwango kikubwa msongamano wa magari jijini Dodoma. Aidha, itasaidia kuunganisha ushoroba wa kati wa nchi na barabara kuu ya Afrika inayotoka Afrika Kusini hadi Misri (Cape to Cairo).

Waziri Ulega aliongeza kuwa mradi huo unakadiriwa kugharimu takriban shilingi bilioni 131 hadi kukamilika kwake. Serikali inaendelea na mazungumzo ya upatikanaji wa fedha za hisani na mikopo nafuu kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo, hususan Benki ya Maendeleo ya Afrika.

​
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ni taarifa Muhimu kwa vyombo vya habari kwenda kwa watanzania wote ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kutoka Ikulu Ya Rais Samia.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Hali ni tete hapa mkoani Simiyu. Raisi Samia atakuwa na ziara hapa.

Sasa maandalizi ya kuonyesha kuwa anakubalika yamekuwa ni maumivu Kwa raia.

Raisi atakapo pita wafanya bihashara wameamliwa kufunga maduka, watumishi wote,Sungusungu ,Mgambo wameamliwa kuhudhuria mikutano ya Samia.

Wenye shule za English medium wameamliwa kutoa magari ya Shule Kwa ajiri ya kusomba raia.

Je hii nguvu kubwa ya Nini, je serikali ya mkoa inawasiwasi kuwa wananchi wanaweza susia mikutano ya Raisi?

Tuombeeni sisi wana Simiyu maana maagizo ni mengi
 
 

Attachments

  • Screenshot_20250614_205425_Instagram.jpg
    306 KB · Views: 36
 
 
Hii ni press release au flier ya kampeni?
 
Mwambie mama yako no reforms no election
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…