Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Chalamila anapokea habari za kutenguliwa akiwa ametokea kwenye ulabu kama alivyopokea siku Magufuli alipofariki.

Mke: Mume wangu umetenguliwa
Chalamila: Aaah mke wangu au ni wewe umepewa talaka? Nieleze vizuri.
 
Chalamila anapokea habari za kutenguliwa akiwa ametokea kwenye ulabu kama alivyopokea siku Magufuli alipofariki.

Mke: Mume wangu umetenguliwa
Chalamila: Aaah mke wangu au ni wewe umepewa talaka? Nieleze vizuri.
Umbea wa kishoga peleka salon.
 
1326.gif

sheed.png
 
Chalamila alizuia Debe letu la Ulanzi wakati 'tunamuaga' Mwendazake pale Mbeya Karma imefanya kazi yake😁
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

=====

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.

Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae
View attachment 1814796
Nimetonywa na watu wakubwa mkoani mwanza,kumbe amesababisha mgogoro mkubwa mkoani,kwani ule kamati nzima ya ulinzi na usalama,mkoani hakuna maaelewano na wamegombana sana
 
Wajapani wana msemo wao... "bilauli ya kwanza mtu hunywa pombe... bilauli ya pili pombe hunywa pombe... bilauli ya tatu pombe hunywa mtu!!" Sikushangaa mkubwa yule alipokengeuka na kusema "...hata rais akitukanwa ni sawa tu!!" Nikajua tayari fyuzi zimeshafyatuka...
Nasikia ni mwalimu wa chuo kikuu. Arudi kushika chaki ukizingatia bado kijana.
 
Mabango mabango na lugha au kauli za ubabe za mwendazake hazina nafasi ktk awamu ya sita. Kiongozi unatakiwa utumie kauli za kushawishi na siyo zitisho n.k.

Tujikumbushe jana RC Chalamila alisema nini :

9 Jun 2021
Mwanza, Tanzania


"MABANGO KWA RAIS SAMIA YAWE NA NIA NJEMA, NITAKULA NAO SAHANI MOJA"— RC CHALAMILA


Mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati akizungumzia ujio wa Rais Samia Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku tatu amegusia suala la Wananchi kujitokeza na mabango mbele ya Rais kuwa yawe na nia njema na wasingoje hadi ujio wa Rais kwani ofisi yake ipo wazi muda wote

Hapo kaongea vitu vya maana Sana kwenye ishu za mabango, labda kama alikua hayo mabango yangemgusa mtangulizi wake.
 
Back
Top Bottom