Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Chalamila alikuwa anahangaika mno. Juzi hapa nimemuona akiwataka wananchi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kwenye ziara ya rais atakayoifanya mkoani humo na akawataka waje na mabango ya kutosha - hata kama ni ya matusi sawa tu. Wakati huo huo mama ameshatoa onyo kuwa hataki kuona mabango wananchi wakiilalamikia serikali; na kwamba mabango hayo yatawa-cost wakuu wa mikoa. Huu ni wakati wa ku-lay low na kusoma upepo unavyokwenda. Haoni wenzake akina Hapi wako kimya wanahamishwa tu huku na huko utafikiri mpira wa kona?
Huu uropokaji ndio umemwondoa alishaonywa huwezi kuwa kiongozi mropokaji Kama vile alitakiwa awaombe Sana mwanza kwa unyenyekevu wajitokeze kumpokea Rais na kuonyesha moyo wa upendo na awaombe kuwa yeye ni mgeni wasimwangushe
 
Hmm…huyu mama naye kama Magufuli tu sasa.

Anateua leo, jioni anatengua.

Kesho anateua, keshokutwa anatengua!

Hivi hao wateuliwa huwa hawafanyiwi vetting??

NB: hizi press releases huwa zinatolewa saa ngapi usiku?
Hivi ungekuwa wewe ungeweza kumuacha mkuu wa mkoa ambaye anahimiza watu waje na mabango hata ya matusi kwenye ziara ya Rais. Chalamila ana hitilafu kwenye ubongo!!
 
Mlevi Chalamila amefanya kosa gani huko?
Tuliandika humu kapelekwa kwenye lango la kutokea asipotuliza akili... wapambe wake wakatubeza Dar na Mwanza ni viatu vikubwa kwa "wenye miguu midogo..." waliokuwa wakimshangilia kwa hizo walizozisifia kuwa ni "akili" nadhani sasa wameelewa "...kwanini ilisemwa pombe kitovu cha uzembe!!" Ati ni comedian.... pole yake twamkaribisha uraiani ambako asipojichunga "wakalimani" watatafuna masurufu na mafao akija tahamaki....
Aione Phillipo Bukililo
Nikinywa pombe na kumaliza chupa ya mwisho huwa sipotezi uwezo wa kufikiria. Kila kitu kikitumiwa kwa kiasi huwa hakina maumivu wala hakileti fedheha.
 

Attachments

  • VID-20210611-WA0027.mp4
    627.1 KB
Hon. Chalamila pitia hapa Mtwara nikupe tendo la ndoa bureee.... upunguze stress, vinginevyo wewe Mnyalu unaweza kujinyonga. Onyo! Usije na hung over ya BALIMI ya Kanda ya Ziwa.

KARAMA imekurudia, Sugu anakusubiri mkanywe ulanzi[emoji846][emoji846][emoji846]
 
Mama Samia kamtengua Chalamila alimuonya kuhusu uropokaji akacheka
 
Hivi ungekuwa wewe ungeweza kumuacha mkuu wa mkoa ambaye anahimiza watu waje na mabango hata ya matusi kwenye ziara ya Rais. Chalamila ana hitilafu kwenye ubongo!!
Tuliandika watu wa "vetting" iko siku watatuwekea mtu atakayefanya "tukio"
 
Kwa nini hatengui teuzi za SIRRO & DIWANI waliokuwa wakisimamia mauji na utekaji wa watz
Hawana muda mrefu ofisini tutegemee wateuliwa hawa wapya wataaapa na wakuu wapya wa vyombo vya ulinzi na usalama, either SIRRO au DIWANI mmoja wao lazma aachie ofisi ndani ya mwezi huu.
 
Mazungumzo ya binti na baba yake usiku huu

Binti: BABA,BABA kuna barua nimeiona mitandaoni, kama inakuhusu
Mkuu wa mkoa: Usiku wote huu, itakua ya mtu mwingine hiyo.
Binti: Baba, mbona nimeona jina kama lako?
Mkuu wa mkoa: Mwanangu aibu hiyo, tuhameni usiku huu huu kabla jua halijachomoza
 
Usiamini maigizo ya wanasiasa. Sasa hivi tupo kwenye bajeti. Wasitutoe kwenye reli!

Hivi kati ya CHALAMILA na mke wa NDUGAI nani hafai? Yule mama alipata hati chafu ya ufisadi Bahi mama kampandisha cheo kuwa RAS Dodoma.

Yajayo yanahuzunisha!
 
Hivi ungekuwa wewe ungeweza kumuacha mkuu wa mkoa ambaye anahimiza watu waje na mabango hata ya matusi kwenye ziara ya Rais. Chalamila ana hitilafu kwenye ubongo!!
Nadhani nimeshalijibu swali lako.
 
Usiamini maigizo ya wanasiasa. Sasa hivi tupo kwenye bajeti. Wasitutoe kwenye reli!.
Hivi kati ya CHALAMILA na mke wa NDUGAI nani hafai? Yule mama alipata hati chafu ya ufisadi Bahi mama kampandisha cheo kuwa RAS Dodoma.
Yajayo yanahuzunisha!
Hii awamu ya sita tusitegemee makubwa na vile rimoti ipo msoga, tugemee kuongezeka kwa watendaji wezi na mafisadi wa kutosha.
 
Back
Top Bottom