Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Wakati mwingine inakuwa rahisi sana kumvizia kiongozi ambaye tayari ana shutumiwa, akiondolewa madai dhidi yake lazima yataibuka hata kama anaweza kuwa ameondolewa kwa sababu nyingine tofauti na zile alizokuwa akishutumiwa nazo, binafsi sijui sababu ya Chalamila kuondolewa, na hakuna ajuae coz hatujaambiwa na mamlaka ya uteuzi.
 
Ally Hapi ndo kwanza alikuwa anajitambulisha kwenye wilaya za mkoa wa Tabora. Jumatatu na Jumanne alikuwa anajitambulisha wilaya ya Kaliua, Jumatano na Alhamisi alikuwa wilaya ya Urambo, Ijumaa amehamishwa mkoa.

Sijui kama alishamaliza kujitambulisha Tabora. Kazi Iendelee.
Si ajabu na huko anakokwenda nako akahamishwa akiwa bado akijitambulisha.
 
Kwa hali tuliyonayo kuna vitu viwili vya kuogopa

Mungu

Technology


Huyo RC inaonekana vyote hivyo hakuwa na hofu navyo

Bahati mbaya vitimbwi vyake vitaendelea kubaki mitandaoni hadi atakapokuwa Mzee na hatimaye wajukuu kuja kumshangaa Babu yao 😅
Aliowaombea watimiziwe ombi la tatu nao wamemwombea aliwe kichwa.
 
Katika Wateuliwa wa4 Wa Leo, Waislam Ni wa3, Mkiristo Ni Mmoja Tu, Rc Wa Mwanza... Twende Tu Tutafika Wakuu
 
Mama pole na majukumu. Nakushauri unapofanya mabadiliko tafuta mtu sahihi kabisa achukue nafasi ya aliyechemsha. Tupunguze ghalama ya uhamisho usio lazima wa watu ili tuepuke ghalama zisizo za lazima. Batlida angeenda Mwanza na DAS Simanjiro angekuwa RAS halafu ungenichukua mtu kama mimi msomi niliyeko kijiweni ukanipa u-DAS Simanjiro.
 
Kwa hali tuliyonayo kuna vitu viwili vya kuogopa

Mungu

Technology


Huyo RC inaonekana vyote hivyo hakuwa na hofu navyo

Bahati mbaya vitimbwi vyake vitaendelea kubaki mitandaoni hadi atakapokuwa Mzee na hatimaye wajukuu kuja kumshangaa Babu yao [emoji28]
Jamaa Kachongewa Na Pm Jana Kwenye Kikao Huko Mwanza
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

=====

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.

Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae

View attachment 1814796

Habari wana JF.
Naomba kujuzwa hivi huyu Batilda Salha Buriani siye yule aliyewahi kuwa waziri na baadaye Balozi wa Tanzania nchini Kenya kipindi cha Serikali ya JK?

Ahsante
 
Mama pole na majukumu. Nakushauri unapofanya mabadiliko tafuta mtu sahihi kabisa achukue nafasi ya aliyechemsha. Tupunguze ghalama ya uhamisho usio lazima wa watu ili tuepuke ghalama zisizo za lazima. Batlida angeenda Mwanza na DAS Simanjiro angekuwa RAS halafu ungenichukua mtu kama mimi msomi niliyeko kijiweni ukanipa u-DAS Simanjiro.
Kweli Mama awafikirie wasomi walioko vijiweni awape teuzi. Hahahhhaa ila hapo neno ghalama sio hivyo bwashee... Ni Gharama
 
Yule jamaa Its either anavuta bangi, unga au pombe kupita kiasi au anajaribu kufanya utani lakini hauwezi utani, anapitiliza mnoo siyo mara ya kwanza kutoa kauli za ajabu.

Kule Mbeya kipindi cha uchaguzi alisema ana hamu na damu za wapinzani kama litre 8 hivi ana mpango wa kuzimwaga, he is terrible.
Terrible,Terrible,Terrible..
 
Back
Top Bottom