Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

=====

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.

Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae

View attachment 1814796
Hamna lolote alikua anamtafutia nafasi batilda buryani tu. 2025 lazima kufanya uamuzi sio hizi show kufurahisha maliberali.
 
Hii inaitwa Chalamila vs bajeti. Je nani ataibuka mshindi?

Kama ilivyokuwa kwa Ndugai vs Sabaya. Na mpaka muda huu Sabaya kaibuka kidedea kwani kafanikiwa kuzima kasi ya kutaka kuwatoa kina Halima Mdee bungeni.
 
Aisee yaan kwenye hili Ametolewa Chalamila tuu peke yake wengine wote wamehamishwa. Sasa na yeye aendelee kula bata na Makonda maana si wote wapo Mwanza au atarudi iringa kupingwa na Baridi.
 
Mama kajua kucheza na akili zetu kote kwa moto. Huku Budget, Huku Chalamila, kule kuna Petition BET
 
Ukiona hivyo ujue na anakesi za kujibu kama Makonda so lazima ajadiliwe Wanambeya watatuambia maana sisi wanaMwanza alikuwa anatuambia Tunywe Pombe.
 
Hamna lolote alikua anamtafutia nafasi batilda buryani tu. 2025 lazima kufanya uamuzi sio hizi show kufurahisha maliberali.
HAPANA KUBWA,sio nyinyi mlio kuwa mnalialia humu mitandaoni eti Chalamila hafai, ukipekua humu JF kuna nyuzi kibao zinapinga uteuzi wa chalamila! au mlikuwa sio ninyi? Haya katekeleza matamanio yenu mmebadiri gia imekuwa anamtafutia mtu nafasi kweli? kweli JF imeingiliwa.
 
Chalamila alikuwa anahangaika mno. Juzi hapa nimemuona akiwataka wananchi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kwenye ziara ya Rais atakayoifanya mkoani humo na akawataka waje na mabango ya kutosha - hata kama ni ya matusi sawa tu. Wakati huo huo mama ameshatoa onyo kuwa hataki kuona mabango wananchi wakiilalamikia serikali; na kwamba mabango hayo yatawa-cost wakuu wa mikoa. Huu ni wakati wa ku-lay low na kusoma upepo unavyokwenda. Haoni wenzake akina Hapi wako kimya wanahamishwa tu huku na huko utafikiri mpira wa kona?
Makeke yakizidi lazima uwaribu, Chalam8la level yake sionkuongoza mkoa
 
Tuanzie hapa,
Kiwanda cha kuchenjuwa nani mmiliki.
Vinginevyo ilikuwa PETROL imemponza
RAHA YA MAMA ANAKULA KICHWA HUKU ANAKULISHA MIKATE NA BURUBENDI.
Hafoki,Bali anakupa msamiati wa kuchekesho.
 
Kwa hali tuliyonayo kuna vitu viwili vya kuogopa

Mungu

Technology


Huyo RC inaonekana vyote hivyo hakuwa na hofu navyo

Bahati mbaya vitimbwi vyake vitaendelea kubaki mitandaoni hadi atakapokuwa Mzee na hatimaye wajukuu kuja kumshangaa Babu yao 😅
Duuh, huyu siyo kiongozi...

Kiongozi kazi yake ni ku - PREVENT na ku - CONTROL uhalifu na wanaokamatwa ni kuacha sheria ivhukue mkondo wake...

RC unapohamasisha watu wajichukulie sheria mkononi kuua kila wanayedhani ni mhalifu, ni KOSA KUBWA, umeshindwa kazi ya uongozi wewe..!
 
Back
Top Bottom