Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni 2021 amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine kama ifuatavyo:-

=====

Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, na kumhamishia mkoa huo Mhandisi Robert Gabriel ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Hatua hiyo imetokana na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo ya wakuu wa Mikoa na kuteua viongozi wengine.

Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Salum Hapi anahamia Mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Batilda Salha Buriani kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora kuchukua nafasi ya Ally Salum Hapi.

Aidha Katibu Twala Wilaya ya Simanjoro Zuwena Omari Jiri ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya Batilda Salha Buriani.

Taarifa hiyo imesema tarehe ya uapisho wa viongozi wapya itatangazwa baadae

View attachment 1814796
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana !
 
Chalamila atenguliwa

Yaan unahitaji kujua nini wakai kila kitu kipo wazi.
Okay hebu fikiria kuwa mama Aliwahi kusema tena BUNGENI kuwa TRA watafute namna ya kukusanya kodi na sio kuwanyanyasa wafanyabiasha kwa utulivu. Alafu Mkuu wa mkoa aliemteuwa yeye anasema Wakatamizwe hauoni hapo hawapo njia moja.

Kingine mama wakati anawaapisha RAC na DC alisema kuwa anataka wakafanye kazi wasiingiliane kwenye majukumu hivyo pia akasema kuwa Wakuu wa mokoa akatoa mfano wa Mwanza tena alisema kuwa kuna BOMU je unategemea nini.

La mwisho alisema hataki kuona watu wanashika mabango ambayo watendaji wakwe wanaweza kutatua kero za hao wananchi alisema Rais. Juzi Chalamila anasema watu wabebe mabango hata kama ni matusi je wewe unazani huyu jamaa alizani yupo na Mwendazake.

Unajua walizoea kuropoka walipokuwa kwa Mwendazake sasa mama sio hivyo. Bora kamtumbua maana hata Mbeya alisumbua sana.
 
Mh. Rais yuko sahihi, Chamila sijui ni ulevi, utani uliopitiliza hayupo serious kazini, unatoa taarifa ujio wa Rais maneno mengi yasiyohusika mara kufukuzwa kazi, mabango ya matusi, nani amewahi andika bango lenye matusi? Watu wabebao mabango wana shida za kweli wewe unafanya utani na dhihaka juu ya kauli ya Rais kuhusu mabango! Mh. Rais yupo sahihi!
Utasemaje yuko sahihi wakati hajatoa sababu za kutengua uteuzi?

Amandla...
 
Wakati watu wanapiga kelele kutaka baadhi ya watu waondolewe kwenye nafasi zao, kuna watu hudhani wanawaonea wivu, ila kwa tukio hili la Chalamila, hata Mama mwenyewe atakuwa amejiunza kwa vitendo.

Kwa msingi huo, namshukuru sana Chalamila kwa kuwa-prove wrong MATAGA na kuthibitisha usahihi wa waliokuwa wanasema kuwa hafai.

Mama pia anapata somo hapa kuwa anapaswa kupokea ushauri hata kama ni wa watu wa mitandaoni au ni wapinzani au wanaharakati.

Bado ataendelea kujionea kwa vitendo.

Muda ni mwalimu mzuri sana.
Tuliwaambia hilo jambo mapema wakatupuuza
 
Ukiachana na Kero ya Kutuongezea Kodi Kwenye Line Za Simu, Kusema Ukweli Mama Anaupiga Mwingi Sana
 
Haingii akilini alijua kabisa Samia hataki mabango bado yeye akasisitiza watu waje na mabango.yani ndio tuseme chalamila yani ameamua kukaidi kwa makusudi.lol
'll be the last one kuamini hii,hii ni movie za kisiasa kama zilivyi movie zingine za kisiasa
 
20210611_095620.jpg
 
Sio watanzania??! Simnasemaga waislamu hawana elimu ndio maana hawateuliwi wengi katika serikali?? Halafu Rais siku zote haangalii dini katika kuteua mtu, Cha Kwanza anaangalia elimu yake ,na je hana record ya jinai, na Ni raia
Tena wengine ni viongozi toka enzi za Mkapa!
 
Aliowaombea watimiziwe ombi la tatu nao wamemwombea aliwe kichwa.
Yaani Mkuu wa Mkoa anakuwa yeye ndiyo hakimu wa kuamua nani aishi na nani auwawe??

Utasema hakuna Mahakama?? Inashangaza hata huo uRC alipewa kwa vigezo vipi🙆🙆
 
Sasa anapelekwa ambako watu hawarembi! Hawana maneno mingi! AKAMAKINIKE! Mara sio Tabora!!!
Huko Tabora wanaroga hatari
Naona Hapi huenda kafurahi kutolewa
Mzee wa fyekelea mbali alikuwa mlokole kapambana sana nao
 
Back
Top Bottom