Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sekiete Selemani

Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sekiete Selemani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Bw. Sekiete Yahaya Selemani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia tarehe 16 Aprili, 2023.

IKUMBUKWE KUWA:
Mwanzoni mwa mwaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'alimshtaki' Mkurugenzi huyo kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni vilivyopo mtaa wa Rwegasore jijini humo.

View attachment 2591994
Ndiyo hii?

Mkurugenzi Jiji la Mwanza ashtakiwa Tamisemi madai ya kuuza viwanja​

Ijumaa, Januari 13, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima
By Anania Kajuni

Muktasari:​

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'amemshtaki' mkurugenzi wa jiji hilo, Sekiete Yahya kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni.

Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'amemshtaki' mkurugenzi wa jiji hilo, Selemani Sekiete kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni.

Wakati barua ya mashtaka ikitua Tamisemi, Malima ameagiza watumishi wanne wa jiji hilo kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa tuhuma za uuzaji wa viwanja hivyo.
Viwanja hivyo namba 194 na 195 vipo mtaa wa Rwegasore jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo Ijumaa Januari 13, 2023, Malima amewataja wanaosimamishwa kazi kwa nyadhifa zao kuwa ni mhasibu wa Jiji, mwanasheria, ofisa manunuzi na ofisa mipango.
Watumishi hao wa umma wanadaiwa kuuza viwanja hivyo vilivyopo mtaa wa kibiashara katikati ya jiji kwa thamani ndogo kulinganisha na bei ya soko.
Amesema walishirikiana kuuza viwanja hivyo bila kufuata utaratibu kinyume cha taratibu na maadili ya viongozi huku mkurugenzi wa jiji akidaiwa kukiuka maagizo ya kamati ya ulinzi Wilaya ya Nyamagana na ofisi ya mkuu wa mkoa.
"Kwa mamlaka yangu nimeelekeza ofisi ya katibu tawala Mkoa wa Mwanza iwasimamishe kazi watumishi wanne ambao ni wakuu wa idara kupisha uchunguzi na tunaandika barua ofisi ya Rais (Tamisemi) kwa hatua kuhusu mkurugenzi wa Jiji," amesema Malima.
Mkuu huyo wa mkoa amesema licha ya suala la maamuzi kuachwa mikononi mwa Tamisemi, mamlaka ya mkoa unaona kuwa kiongozi huyo amekosa sifa za kuendelea kusalia mkoani humo.
Ameagiza idara ya ardhi kuangaliwa upya pamoja na watumishi hao wanne kuchunguzwa endapo wamehusika katika tukio hilo.
Maazimio ya kikao cha Ulinzi na Usalama wilaya ya Nyamagana Septemba 28, 2022 ilikataza kurejesha au kufanya uwekezaji wowote wa viwanja vitano kuanzia namba 191 hadi 196 bila kamati hiyo kufahamishwa.
 
Kama tuhuma ni za kweli, inabidi sasa afikishwe mahakamani.
Afikishwe mahakamani tena! Labda kama alikula peke yake.

Kwani wale wa kuongeza cha juu kwenye ununuzi wa ndege ya mizigo, wamefikishwa mahakamani?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Bw. Sekiete Yahaya Selemani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia tarehe 16 Aprili, 2023.

IKUMBUKWE KUWA:
Mwanzoni mwa mwaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'alimshtaki' Mkurugenzi huyo kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni vilivyopo mtaa wa Rwegasore jijini humo.

View attachment 2591994
Sasa mbona haisemi kesho asubuhi akaripoti ofisi gani! Kwahiyo atakaa nyumbani akisikiliza chaneli na stesheni zote za vyombo vya habari kama atatajwa kwenye nafasi nyingine.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Bw. Sekiete Yahaya Selemani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia tarehe 16 Aprili, 2023.

IKUMBUKWE KUWA:
Mwanzoni mwa mwaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'alimshtaki' Mkurugenzi huyo kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni vilivyopo mtaa wa Rwegasore jijini humo.

View attachment 2591994
hizi mambo za kuteuliwa, ni ngumu sana, si ukute mtu aliacha kazi yake akatii uteuzi, anatenguliwa halafu anaishije sasa? ndo maana wengine wanakataa.
 
Na ramadhani hii yote ya kumi la msamaha kwa ALLAH kweli swaumu za hao waliomtengua zitashihi kweli........
Nchi inaendeshwa kwa sheria zake utumishi na katiba na sio kwa sheria za Ramadhani au futari!
Tusichanganye mambo
 
Back
Top Bottom