Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sekiete Selemani

Rais Samia atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sekiete Selemani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Bw. Sekiete Yahaya Selemani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia tarehe 16 Aprili, 2023.

IKUMBUKWE KUWA:
Mwanzoni mwa mwaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'alimshtaki' Mkurugenzi huyo kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni vilivyopo mtaa wa Rwegasore jijini humo.

View attachment 2591994
DED wa Arusha mbona hatenguliwi na Kuna Ufisadi Kila siku unaripotiwa na Gambo?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Bw. Sekiete Yahaya Selemani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia tarehe 16 Aprili, 2023.

IKUMBUKWE KUWA:
Mwanzoni mwa mwaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'alimshtaki' Mkurugenzi huyo kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni vilivyopo mtaa wa Rwegasore jijini humo.

View attachment 2591994
Pesa za Umma zirudishwe,

Tengua, Tenga haisaidii chochote.
 
hizi mambo za kuteuliwa, ni ngumu sana, si ukute mtu aliacha kazi yake akatii uteuzi, anatenguliwa halafu anaishije sasa? ndo maana wengine wanakataa.
Cheo cha umma ni dhamana. Kabla yake alikuwepo mwingine na anayekuja ataondoka na atakuja mwingine. Muhimu ukiaminiwa na mamlaka ya juu ya nchi au ukifanya kazi kwa nafasi yoyote ya umma lazima uwe mwadilifu na mzalendo kwa taifa lako.# Usiwe na tumbo lisilokinahi na bahari ya uchu🙏🙏🙏
 
Uzuri wa mama huwa hakurupuki....ila akijiridhisha tu ujue umekwisha..........

Kumbukeni katoa maelekezo kwa watendaji wote waisome ripoti ya CAG 2021/2022
Mkuu, tatizo kubwa tulilonalo hapa kwetu TZ ni kwamba akija mtawala mwingine anamrudisha tena madarakani. Wasomi wapo wengi sana, mtu akitenguliwa ama akionja assli ya uhuru na akitenguliwa, asiajiriwe tena Serikalini. Hii itasaidia sana, watumishi wa Umaa kuwa makini katika utendaji wao wa kazi.
 
MSIDHANI AKITENGULIWA NDO HALI MSHAHARA. HAPO MSHAHARA UPO KAMA KAWA
nafasi za kisiasa ukitenguliwa ndio basi labda kama ulikua na kazi serikalini unarudi kwenye kazi yako ila kama ni kada ulikua jobless basi tena na mshahara unayayuka unakua kama kina hally heppy unarudi kulima
 
Mkuu, hapo yupo kazini; swaumu haihusiami na masuala ya kazi.
lakini je nauyo anayemtengeua nayeye hana madhaifu katika utendaji wake wa kazi,ama yeye kama mkuu wa nchi katiba inamlinda hagusiki
 
Huyu Bw Sekiete alitoka Nzega DC hadi Mwanza CC!

Sijui alifanya maajabu gani hapo Nzega hadi akapelekwa jijini.
Ajabu ya nchi hii ipo siku utasikia amepewa tena kitengo sehemu nyengine japokuwa ameshaonekana makosa yake.

Mimi hadi huwa nawaza kwani huwa hakuna watu wengine hata walio nje ya system ya serikali wanaostahiki hizo kazi kiasi kila siku wawe walewale hata waliokwisha kutuhumiwa kwa ubadhirifu?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Bw. Sekiete Yahaya Selemani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia tarehe 16 Aprili, 2023.

IKUMBUKWE KUWA:
Mwanzoni mwa mwaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima 'alimshtaki' Mkurugenzi huyo kwa Wizara ya Tamisemi ambayo ndio mamlaka yake ya nidhamu, akimtuhumu kuhusika na uuzaji wa viwanja viwili vyenye thamani ya Sh1 bilioni vilivyopo mtaa wa Rwegasore jijini humo.

View attachment 2591994
Na hapo Rais kamaliza kazi!
Mheshimiwa Sekiete atapangiwa kazi nyingine.

Sasa huu tuuite "ujinga" au "upumbavu"? ama kuna jina jingine linaloeleza vizuri hatua za namna hii ndani ya nchi?
 
Back
Top Bottom