Rais Samia atengua Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya za Temeke na Kilindi

Rais Samia atengua Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya za Temeke na Kilindi

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Julai, 2023 amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:

1) Ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Pia, soma: Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

2) Ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama. Amemhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Hashim Shaib Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.

3) Amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini.

Screenshot 2023-07-02 at 23.29.32.png
 
Hii mbinu haiwezi kuhamisha mjadala uliopo, ni mbinu ya kijinga..., tunataka vipengele vya mkataba vya kuiuza Tanganyika virekebishwe
Wanaokutumia saa hizi wamelala. Ngoja waamke wakutumie mengine uandike.
 
Mwacheni Rais afanye kazi yake. Anapitia taarifa nyingi. Hao wawili wanaweza kuwa na matatizo yako.
Endelea President.
 
Mtu kashalala saa hizi kapasiwa na nguo za kesho za kazini, anamka asubuhi akiwa anamsubiria dereva wake aje amchukue anashangaa kupata breaking news kuwa katumbuliwa
Wewd ndio ni unamawazo hayo lakini kabla ya mtu kuteuliwa huwa anajulishwa kwanza na kuna makaratasi anasaini kukubali uteuzi, vivo hivyo kwa anaetenguliwa taarifa anapewa hata kabla haijawa public.
 
Wanaokutumia saa hizi wamelala. Ngoja waamke wakutumie mengine uandike.
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Samia ana dharau jamani. Kaji kutoka kamishina wa Taasisi ya kuzuia madawa ya kulevya hadi kuwa mkuu wa wilaya. Hatareee. Angempa walau ukuu wa mkoa au ukurugenzi wa mkoa basi.
 
Wewd ndio ni unamawazo hayo lakini kabla ya mtu kuteuliwa huwa anajulishwa kwanza na kuna makaratasi anasaini kukubali uteuzi, vivo hivyo kwa anaetenguliwa taarifa anapewa hata kabla haijawa public.
Acha uongo. Mwigulu alitenguliwa akiwa Kigoma huko bila taarifa wala nini.Wale viongozi wa chama cha walimu si juzi tu wamegomea ukuu wa wilaya na majina yalikuwa tayari mkekani.
 
Sasa huyu mkuu wa wilaya ya Tanga ,naona kama ni demotion kutoka kuwa kamishina wa kupambana na madawa ya kulevya mpaka wilayani? Hadhi yake ni sawa na IGP,Cdf,CGi
 
Back
Top Bottom