Rais Samia atengua Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya za Temeke na Kilindi

Rais Samia atengua Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya za Temeke na Kilindi

Ilikuwa style ya Magu ya kukupima unyenyekevu wako, Diwani alitolewa DCI akafanywa RAS akakaaa kimyaaaa miezi michache baadae akwa DG TISS
Ila mama alipomtoa hapo kwenye DG TISS na kumpeleka Ikulu kama Katibu ikawaje?😀😀
 
Ila mama alipomtoa hapo kwenye DG TISS na kumpeleka Ikulu kama Katibu ikawaje?😀😀
Pale nahisi kamtega , hamwamini sana kuiongoza TISS lakini hataki kumweka mbali kutokana na ujuzi wake na umri bado sana , Na jamaa ni very resoursefull ila mkimya sana mpaka anawaogopesha wakubwa . ( Hayo mawazo yangu tu kwa ninavyomfahamu kidogo enzi yupo polisi hakuna mtu aliwahi kuhisi jamaa yupo state dept)
 
Daah, hatari, ila..

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Samia ana dharau jamani. Kaji kutoka kamishina wa Taasisi ya kuzuia madawa ya kulevya hadi kuwa mkuu wa wilaya. Hatareee. Angempa walau ukuu wa mkoa au ukurugenzi wa mkoa basi.
Ndiyo changamoto hizo uzuri mshahara wake mkubwa kama boss huko tiss anaendelea kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya ni bonus
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 02 Julai, 2023 amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:

1) Ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Athumani Munkunda na kumteua Mobhare Holmes Matinyi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

2) Ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Yeji Busalama. Amemhamisha kituo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini, Hashim Shaib Mgandilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi.

3) Amemteua James Wilbert Kaji kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini.

View attachment 2676676
Kama huyu James Wilbert Kaji ni yule wa TISS aliyewahi kuwa PSU kabla ya kwenda Mbeya kuwa ama RSO au DSO kisha akaja kuwa Kamishina Mkuu wa DCEA na Kuharibu mno huku akichukiwa na Watendaji wengi na akiwa na Sifa Kuu ya Ujeuri na Dharau kwakuwa alikuwa anatokea Mkoa na Eneo atokalo Hayati Magufuli na wana Undugu nae ndiyo Kateuliwa na Mheshimiwa Rais Samia sasa taratibu GENTAMYCINE naanza Kuamini Utawala huu wa sasa una Mapungufu makubwa yanayoelekea Kuihatarisha nchi na Ustawi wake Siku si nyingi.

Nimesikitika sana na mno. Kazi ipo!!!
 
Back
Top Bottom