Rais Samia atengua Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya za Temeke na Kilindi

Acha uongo. Mwigulu alitenguliwa akiwa Kigoma huko bila taarifa wala nini.Wale viongozi wa chama cha walimu si juzi tu wamegomea ukuu wa wilaya na majina yalikuwa tayari mkekani.
Komaa na komwe lako
 
Ingekuwa enzi za JPM alikuwa anasema sababu ya kukutengua, maana hata aliyekuwaga DAS wa Kisarawe wakati anamtengua alisema sababu kuwa ni kutembea na wake za watu

Ila Madam President hajawahi kusema
 
Wewd ndio ni unamawazo hayo lakini kabla ya mtu kuteuliwa huwa anajulishwa kwanza na kuna makaratasi anasaini kukubali uteuzi, vivo hivyo kwa anaetenguliwa taarifa anapewa hata kabla haijawa public.
Mwigulu wakati anatumbuliwa na Jiwe ulikuwa bado hujaja Tanzania? Kangi Lugola je?
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Ndio maana nikasema kwamba wewe unatumiwa na wakwepa ushuru wa bandarini, wapitisha madawa ya kulevya na wezi wa vifaa vya magari na vitu mbali mbali vilivyopo pale bandarini.

Haiwezekani mtu mwenye akili yako huru na ambayo haijawekwa mfukoni na mtu yoyote utoe tuhuma bila kuweka ushahidi wa kile unachokituhumu afu utegemee mtu mwenye akili timamu kama mimi nitaungana na wewe kupigania masilahi ya wajanja wachache niliowataja hapo juu.

Weka mkataba wote hapa tuangalia hayo uliyoyaandika hapa kama yana ukweli kwa faida ya wasomaji wote.

Mimi sio mtu wa kuandikiwa au kuambiwa tu vitu na mtu au mwanasiasa fulan na mimi nianze kupanua mdomo bila kuoneshwa ushahidi, kwa faida yake yeye na familia yake.

Weka huo mkataba hapa tuone haya uliyoyaandika na kama hauna basi nitaamini kuwa na wew ni miongoni mwa waliolishimwa matango pori na wanufaika wa bandarini.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Mpaka kielewe katika sauti ya Freeman Eikael
 
Hawa wakuu wa Wilaya za Kilindi na Temeke wamekosea wapi tena ..si teuzi za juzi tu hapa...???

Halafu huyu Mobhare si tuliambiwa humu na wajuvi wa nchi hii kwamba ni moja ya Senior Officers na wenye nafasi pana pale kwa Mtakatifu 'Peter'...nae kaunguza nn ... hadi kupelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya?

Tumeshazoea Wakazi wa pale ... mara nyingi huenda kuwa RAS wa huko nyanda za linakozama jua...whats happened kwa huyu Mnene!!!

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuboresha safu ya utendaji kazi kwa kufanya mabadiliko madogo katika nafasi za Wakuu wa Wilaya kama ifuatavyo:-
IMG-20230702-WA0005.jpg
 
Ni jambo jema,

Turudi kwenye mjadala kuhusu Bandari 🙏🙏🙏
 
Huyu James kaji toka kamishna wa kupambana na dawa za kulevya mpaka ukuu wa wilaya
 
Back
Top Bottom