BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mara kadhaa imekuwa ikizungumzwa kuwa wawili hao ni mtu na mkwewe lakini hakuna kati yao aliyewahi kuzungumzia hilo.
Akiwa safarini leo Septemba 20, 2023 kutoka mkoani Lindi Rais Samia amesimama wilayani Rufiji na kuwasalimia wananchi waliokuwa wamejipanga barabarani kusubiri msafara wake.
Baada ya Mchengerwa ambaye ni Mbunge wa Rufiji na mawaziri wengine kupata fursa ya kuwasalimia wananchi ikafika zamu ya Rais Samia na ndipo alipoeleza hilo japo kwa mafumbo.
“Nilikuwa safarini lakini isingewezekana kupita Rufiji bila kusimama, nina Vichengewa viwili nyumbani kwangu sasa siwezi kupita nisisalimie wajukuu, ndiyo maana nikasema nisimame niwasalimie wajukuu,” amesema.
Rais Samia ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wakazi wa Rufiji hasa vijana kujikita kwenye kilimo cha mpunga kwa kuwa sasa ni zao la biashara.
“Mpunga imekuwa zao la biashara hivyo niwasihi wakazi wa Rufiji hasa vijana ingieni kwenye kilimo hiki. Mshiriki kwenye mradi wa BBT tulime mpunga kwa wingi ili tuweze kuuza nje,” amesema Rais Samia.