Rais Samia athibitisha uhusiano wake na Waziri Mchengerwa

Rais Samia athibitisha uhusiano wake na Waziri Mchengerwa

Ukiuliza pesa iliyomwangwa hapo ndo utashangaa ya Mchengelwa na Mama mkwe wake, leo nataka niwambie kwa mfumo za tawala za kafrika ,Mchengelewa ananguvu sana kuliko waziri yoyote , thats

Unaweza msikiliza matamshi yake huingilia mpaka wizara isiyo mhusu ya mambo ya ndani,

Ila Mungu anasema na narudia kwa kua utawala wa ccm alisha ufutwa ,hata wawepo mchengelwa 100, uchaguzi ukifanyika hatakuja hamini macho yao,ilisha kua asema Bwana
Dua la kuku halimpati mwewe.
 
Alikosa muda wa kujibu Kero za Mwananchi kwamba aongee na Wabunge / Wawakilishi ila ana muda wa hizi Porojo ?
 
Kama ulikuwa unasikia tu basi leo Rais Samia Suluhu Hassan amethibitisha uhusiano wake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mohamed Mchengerwa.

Mara kadhaa imekuwa ikizungumzwa kuwa wawili hao ni mtu na mkwewe lakini hakuna kati yao aliyewahi kuzungumzia hilo.

Akiwa safarini leo Septemba 20, 2023 kutoka mkoani Lindi Rais Samia amesimama wilayani Rufiji na kuwasalimia wananchi waliokuwa wamejipanga barabarani kusubiri msafara wake.

Baada ya Mchengerwa ambaye ni Mbunge wa Rufiji na mawaziri wengine kupata fursa ya kuwasalimia wananchi ikafika zamu ya Rais Samia na ndipo alipoeleza hilo japo kwa mafumbo.

“Nilikuwa safarini lakini isingewezekana kupita Rufiji bila kusimama, nina Vichengewa viwili nyumbani kwangu sasa siwezi kupita nisisalimie wajukuu, ndiyo maana nikasema nisimame niwasalimie wajukuu,” amesema.

Rais Samia ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wakazi wa Rufiji hasa vijana kujikita kwenye kilimo cha mpunga kwa kuwa sasa ni zao la biashara.

“Mpunga imekuwa zao la biashara hivyo niwasihi wakazi wa Rufiji hasa vijana ingieni kwenye kilimo hiki. Mshiriki kwenye mradi wa BBT tulime mpunga kwa wingi ili tuweze kuuza nje,” amesema Rais Samia.
Hii picha ni kabla hajawa rais au ni baada?
Maana haiwezekani mbunge/waziri kuvaa tai nyekundu mbele ya rais! Ni kinyume na protocol
 
Pmj na kuwa na uhusiano ila mchengerwa Ni waziri makini Sana na boraa Basi tu wakina nape wakiwa ndio washkaji zake atapotea ila mchengerwa Ni waziri Bora Sana na mchapakazi
 
Charity begin at home ,wangapi wanatoa fursa Kwa ndugu na jamaa wa karibu wakiwa katika nafasi Fulani ? Mmesahau mambo ya mtoto wa dada kuwa kwenye chungu HAZINA ?
 
Ni haki yake kupita kusalimia wajukuu

Na mtoto hasa wa kike huwezi mpangia aolewe na nani hata ujifanye mzazi jeuri vipi atajioza atazaa juu kwa juu meza Wembe kama wewe mzazi jeuri

Mtoto kaamua kuolewa na Mrufiji mama Hana cha kufanya hata kama yeye Raisi angeweza muoza kwa wapemba wenye mapesa hatari .Lakini ndio hivyo uamuzi wa mtoto Wa kike atafanyaje

Kazi yake sasa Zaidi ni ya kuhakikisha tu wajukuu.wanaishi vizuri
 
Back
Top Bottom