Rais Samia atoa mabilioni ya fedha sekta ya anga, elimu, mradi wa SGR na bwawa la kufua umeme la mwalimu Nyerere

Rais Samia atoa mabilioni ya fedha sekta ya anga, elimu, mradi wa SGR na bwawa la kufua umeme la mwalimu Nyerere

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301


RAIS SAMIA ATOA MABILIONI YA FEDHA SEKTA YA ANGA, ELIMU, MRADI WA SGR NA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MWALIMU NYERERE.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan aendelea na utekelezaji wa ufunguaji na ukuzaji wa uchumi wa Tanzania kwa kutekekeleza miradi ya kimkakati kwa kasi ya ajabu.

Kufuatila ripoti ya Msemaji Mkuu wa Serikali (Habari Maelezo), Mhe. Gerson Msigwa amasema kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imekwishalipa takribani shilingi bilioni 212.959 kwa ajili malipo ya awali ya ununuzi wa ndege nyingine tano.

Pia Rais Samia ametoa Bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kasi (SGR) kuhakikisha mradi huo wa kimkakati unaendelea na kumalizika kwa wakati.

Msigwa aliongeza kuwa Rais Samia pia katoa Bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere uliopo Mto Rufiji, Bilioni 20 kwa ajili ya utoaji elimu bure kwa watoto wa Kitazania na Bilioni 55.4 nyingine kwa ajili ya ujenzi wa Barabara.

Mbali na miradi hiyo ya kimkakati, *Rais Samia pia ametoa mabilioni ya fedha kutekeleza huduma za kijamii kama Umeme Vijijini (REA) na ununuzi wa nafaka.

#TwendePamoja #KwaMatokeoYaHaraka
 


RAIS SAMIA ATOA MABILIONI YA FEDHA SEKTA YA ANGA, ELIMU, MRADI WA SGR NA BWAWA LA KUFUA UMEME LA MWALIMU NYERERE.
Hivi mkiandika hivi hamuoni mnapotosha watu. Hapo ni kama vile anatoa hela yake mfukoni kumbe sio hivyo.

Ni sawa na mnaosema "serikali ya mama samia au serikali ya rais fulani". Msiwamilikishe hawa watu nchi kizembe.
 
Wale waliokuwa wanapiga mahesabu ya kutafuna hela hizi kupitia vikao vya katiba watafute njia nyingine ya kujitafutia riziki za halali. Hizi hela mama aendelee kuzipeleka katika mambo ya msingi kama haya. Wanaotaka katiba waiweke katika ilani yao ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Hakuna tena mamilioni ya kwenda kula bata Dubai na Africa kusini.
 
Kuhusu kununua hizo ndege ni kuendelea kutumia vibaya kodi za wananchi
 
Tayari kuna mashirika mengine mengi ya ndege yanahudumia

Afanye mpango awarudishe na fastjet

Serikali haina sababu yoyote ya msingi ya kununua ndege kwa sasa sababu waTanzania wengi hilo siyo hitaji lao la msingi
 
Ni sawa na kusema Pohamba atoa Pesa ya kununua Sukari kwa Familia yake

Inakuwa habari nisipotekeleza Jukumu langu sio vinginevyo

Mwendelezo ule ule wa kukuta Breaking news TBC Rais azindua Soko
 
Kama ningebahatika kuwa rais basi Serikali yangu ingekuwa bize na mambo ya ulinzi, jeshi na kodi

Mengine yote ningeachia sekta binafsi
 
Duh!Ana hela nyingi kweli!Atakuwa ana mshahara mnono "kwerikweri"!Anigawie na mimi.
 
Nimeelewa hapo uliposema kuwa Serikali imetoa bilioni kadhaa kwaajili ya ununuzi wa ndege.

Sijaelewa uliposema Rais Samia ametoa bilioni 50 kwaajili ya bwawa na nyingine tena bilioni 50 kwaajili ya SGR. Unamaanisha hiyo hela imetolewa na yeye binafsi, familia yake au wamemchangia wananchi wa Mchambawima ili ije kusaidia miradi ya huku bara?
 
Hivi kwa nini Matanzania tunakuwa mapumbavu hivi? Huyo ana hela gani ya kutoa? Sema serikali imetoka fedha!
 
Ni muhimu tuelezwe kikao cha Bunge la Bajeti lilipanga bajeti ya nchi gani au ya shughuri gani, na pesa walizozipanga zimepelekwa nchi gani na hizo anazotoa Rais zinatoka wapi!
 
Hivi mkiandika hivi hamuoni mnapotosha watu. Hapo ni kama vile anatoa hela yake mfukoni kumbe sio hivyo.

Ni sawa na mnaosema "serikali ya mama samia au serikali ya rais fulani". Msiwamilikishe hawa watu nchi kizembe.
Wenzako wanampigia kampeni za siku za usoni kijanja wewe unawawekea kauzibe

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Hizi pesa anazotoa Samia, ni kutoka wapi? Mbona sisikii kelele za kuuliza kama zilipitishwa bungeni? Au ni kutoka mwenye mshahara wake?

Huyu anayefuata sheria, anawezaje kulipinga bunge? Naam, kinadharia, wameleta maombi ya jinsi ya kutumia pesa za umma, tukawakubali kwa jinsi walivyoomba, pengine kukiwa na maboresho kidogo. Sasa kwenye utekelezaji, kwanini hawa vilaza(PM, Gwajiboy n.k) akiwemo, aseme Samia katoa hichi, Samia katoa kile?

Ina maana anayo mamlaka ya kubatilisha mautumizi tuliyoidhinisha?
 
Back
Top Bottom