Rais Samia atoa pole kufuatia mauaji Daraja la Salender, ataka uchunguzi ufanyike

Rais Samia atoa pole kufuatia mauaji Daraja la Salender, ataka uchunguzi ufanyike

Yule jamaa ambae Serikali inamwita kuwa ni "gaidi" hana uwezo wa kuua Polisi.Lile tukio ni staged event.Limepangwa na muda siyo mrefu Serikali itaanza kujiumbua yenyewe kwa sababu hawajawahi kuwa na akili katika kupanga matukio.
 
Yule jamaa ambae Serikali inamwita kuwa ni "gaidi" hana uwezo wa kuua Polisi.Lile tukio ni staged event.Limepangwa na muda siyo mrefu Serikali itaanza kujiumbua yenyewe kwa sababu hawajawahi kuwa na akili katika kupanga matukio.
 
Tukio hili lililotokea tarehe 23/8/2021 nchini KNY lilitosha kutoa taadhari (RED FLAG) kwa wanausalama. Inaonyesha Magaidi yamejipanga kuleta mtafaruku katika ukanda huu wa EA. Baadhi ya wasomali waliopo/wanaoingia nchini ni wa kuchukuliwa kwa taadhari kubwa sana haswa ikizingatiwa Somalia imeonekana kuwa na kambi za mafunzo ya Ugaidi kwa muda sasa. Inahitajika uchunguziwa kina kuhusu watu hawa.
https://citizentv.co.ke/news/two-terror-suspects-arrested-at-likoni-ferry-crossing-in-mombasa-13097443/
 
Salamu zake ni hizi:

Natoa pole kwa Jeshi la Polisi na familia za Askari 3, na Askari 1 wa kampuni ya ulinzi ya SGA waliopoteza maisha baada ya mtu aliyekuwa na silaha kuwashambulia katika eneo la Salenda, Dar es Salaam.

Mtu huyo amedhibitiwa na hali ni shwari. Nawaagiza Polisi kuchunguza kwa kina.


View attachment 1908144

PIA, SOMA:
- Kinondoni, Dar: Mtu asiyejulikana, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Anaagiza kutokea Twitter[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Binafsi najiuliza ujasiri na zaidi utulivu wa hao raia waliorekodi hili tukio.
Nawapongeza watanzania wa maofisini na barabarani maeneo hayo
Mana tumepata movie kamili kwa angle mbalimbali watsap

ila siku nyingine mjilinde kwanza jmn
Stanbic risasi zimepita dirishani live
 
Naomba niongezee kutoa pole kwa familia ya jambazi pia
Tumempoteza mtu jasiri
Anayeweza kuwapa askar wetu mafunzo kwa vitendo [emoji16][emoji16]
Kwahiyo manjagu walikuwa field, alafu wamefeli au siyo.
 
Leo Tumepata Video Kwa Kila Angle! Sasa Unajiuliza Tukio La "Tundu Lissu" Halikupata Video Hata1?
 
Tunashukuru kwa salamu, lakini yeye kama rais anatakiwa ajitathimima na kusahihisha palipo na makosa, ingawa amepokea nafasi ya uongozi bila kuwa na matarajio na kwenye changamoto lakini ni muhimu kujisahihisha panapo stahili, matumaini Mungu atamfanyia wepesi amalize kipindi chake kwa heri.
 
Kwa tabia za polisi tz am sure kuna wengi wamefurahi

Ni mawazo yako ya kijinga tu

Ila huwezi kufurahi polisi kuuliwa/

Polisi ni mtanzania mwenzako anaweza kuwa baba ako,binamu,mjomba au hata rafiki yako.

Jaribu kuwa na akili japo ndogo yakufikiria police hawatoki nje ya tanzania ni hawa hawa ndugu Zetu
 
Karekodi Mwanaume wa Kanda ya ziwa.

Nyie wadasalama mlikua mmejificha.

Kuna wanaume..na kuna wanaume wa Kanda ya ziwa ambao maisha ya risasi. Mabomu, walishayazoea.

Naona unafanya utani na risasi ww, kanda ya Ziwa ndio wamezoea risasi? Hivi ukiwa unaandika unajitoa ufahamu n kuonyesha how poor minded you are, tatizo practically hujui hata maana ya risasi.
 
..unakumbuka Maza alisema askari wa ccm wanaua kwa risasi zisizozidi tatu?

..sasa huyu gaidi wa leo mmeona risasi ngapi zimetumika pale?
Hili nimeshangaa kweli kweli yani huyo jamaa alikuwa kasimama barabarani peupe kabisa lakini polisi walimfyatulia risasi karibu 20 ndo wakampata na akadondoka chini....!
 
Tukio hili linanirejesha kwa kilichomtokea Tundu Lissu.

Nani aliondoa ulinzi area D? Walinzi wangekuwepo bila shaka wangepambana na magaidi waliomshambulia Lissu.
Mnatafuta Kila upenyo muweke agenda zenu
 
Back
Top Bottom