Rais Samia atoa TZS 300BL kukamilisha majengo ya Serikali Jijini Dodoma

Rais Samia atoa TZS 300BL kukamilisha majengo ya Serikali Jijini Dodoma

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
2,823
Reaction score
2,466
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa jumla ya TZS 300BL kwaajili ya kukamilisha safari ya Serikali kuhamia Jijini Dodoma,

Waziri mkuu wa Tanzania Majaliwa Khasim Majaliwa amesema jumla ya magorofa 20 yatajengwa na Serikali na mengine 4 yatajengwa na Sekta binafsi.

Akizundua awamu ya Pili ya Ujenzi wa nyumba za Serikali Waziri Mkuu ameoneshwa kuridhishwa na namna Ujenzi unavyoendelea.

Mpaka Sasa Serikali imetumia jumla ya TZS 168BL na imetoa ajira 1,588.


Source : UTV Habari
 
Wakati ndugu James Mbatia anaendelea kuropoka ,Serikali adhimu ya mh.SSH inaendeleza kazi iliyowashinda tawala nyingi nyuma juu ya kulijenga jiji la Dodoma.. ...

#Kazi Inaendelea kwa Kasi & Weledi zaidi 💪
201101q.jpg
 
Sekta binafsi kujenga gorofa 4 pekee huku serikali ikijenga gorofa 20 inaonyesha jinsi sekta binafsi ilivyo hoi bin taaban........ilitarajiwa kama serikali imejenga gorofa 20, sekta binafsi ziwe 80....
 
Kama hizo taarifa katoka matelephone majaliwa naomba tupuuze tu hajawai kua na data zenye proof
 
Kazi anayotufanyia huyu Mama kwakweli Mungu azidi kumbariki na ninamuombea sana Mungu amlinde dhidi ya mabaya yote yamuepuke.

Amen.

# Tunakupenda sana Mama yetu SSH.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa jumla ya TZS 300BL kwaajili ya kukamilisha safari ya Serikali kuhamia Jijini Dodoma,

Waziri mkuu wa Tanzania Majaliwa Khasim Majaliwa amesema jumla ya magorofa 20 yatajengwa na Serikali na mengine 4 yatajengwa na Sekta binafsi...
Kaziiendelee Mama yetu
 
Ametoa 300B sio na ajira! Hizo ajira ziendelee hata baada ya Majengo kukamilika basi
 
Back
Top Bottom