Ze Bulldozer
JF-Expert Member
- Jun 12, 2020
- 1,070
- 568
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATOA TZS 35BL KUJENGA UWANJA WA "MUSOMA AIRPORT " ILI KUMUENZI HAYATI BABA WA TAIFA KWA VITENDO.
Serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu Hassan imesema inatarajia kutumia kiasi cha TZS 35BL ili kuboresha uwanja wa ndege wa Musoma uliotelekezwa na awamu zote tangu Uhuru,
Maboresho hayo ni pamoja na kuweka lami na kuongeza urefu wa uwanja huo ili kuruhusu ndege kubwa na ndogo kuweza kutua mkoa wa Mara. Uwanja huu pia utahudumia na maeneo ya jirani kama Simiyu na Mwanza,
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Musoma|Mara na pia kuchochea biashara ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo mkoani humo kwani kabla Watalii wengi walishuka uwanja wa KIA,
Ameongeza kuwa Uongozi wa Wilaya tayari umejipanga kwa kuupokea mradi huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkandarasi huyo kwa kumpatia eneo la kuchimba mchanga na kokoto za ujenzi.
Naye, Meneja wa Uwanja wa ndege wa Musoma, Mohammed Bakari, amesema kuwa uwanja huo utajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Beijing kutoka China na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.
Amefafanua kuwa Mkandarasi huyo tayari ameshawasilisha vifaa vyake katika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo, na kusisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mara.Hakika hakuna kama Rais Samia Suluhu Hassan,