Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa

Cheap!
Kumuenzi Mwalimu Nyerere kiuhalisia ni kumaliza Bwawa la Nyerere hilo lilikuwa ni wazo lake na kuhamia Dodoma, Nyerere alianzisha Mji Mkuu mpya wa Dodoma.

Yote mawili Bwawa la Nyerere na Dodoma Samia anayapiga vita, kama si kwa maneno basi kwa vitendo, angalau kulingana na matendo ya watendaji wake.
Mengine yote usanii tu.
Samia ametoa ni pesa ake mfukoni? hizi kodi za wananchi mbaya zaidi yeye hashiriki kulipa kodi mshahara wake haukatwi kodi. Ni dharau kubwa sn kwa wananchi
Kwa hiyo kuboresha Uwanja wa Ndege wa Musoma, alikozaliwa Mwalimu sio kumuenzi? Mwendazake alifanya unafiki mkubwa kwa kutoanzisha mradi wowote mpya mkoani Mara, japo alikuwa anajifanya anamuenzi Mwalimu. Mradi pekee aliowazuga watu wa mkoa wa Mara ni kukamilisha (sio kujenga) mawodi mawili matatu ya akinamama wajawazito na watoto kwenye hospitali ya Kwangwa, Musoma zaidi ya hilo hakuna. Hata mradi wa maji wa Bunda aliukuta ukiwa unaendelea tangu enzi za Kikwete. Mama kaamua kutengeneza airport ili kufungua njia nyingine za kiuchumi ikiwemo utalii maana wazungu wakishuka Musoma ni rahisi kwenda Serengeti
 
Mkuu sami huo uwanja kaja kukamilisha tu mradi umeanza enzi za jiwe maan ata fidia watu wamelipwa wakat wake
 
BILIONI 35 KUJENGA UWANJA WA NDEGE MUSOMA KUMUENZI BABA WA TAIFA KWA VITENDO,​

3-25.jpg

Huu ni muonekano wa baadhi ya vifaa vya ujenzi vya mkandarasi Beijing kutoka nchini China ambavyo vinatarajiwa kutumika katika kazi za maboresho ya uwanja wa ndege wa Musoma sehemu aliyozaliwa muasisi wa Taifa hili,

Serikali ya Rais Samia Suluhu imesema inatarajia kutumia kiasi cha TZS 35BL ili kuboresha uwanja wa ndege wa Musoma,

Maboresho hayo ni pamoja na kuweka lami na kuongeza urefu wa uwanja huo ili kuruhusu ndege kubwa na ndogo kuweza kutua.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Musoma na pia kuchochea biashara ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo mkoani humo.

Ameongeza kuwa Uongozi wa Wilaya tayari umejipanga kwa kuupokea mradi huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkandarasi huyo kwa kumpatia eneo la kuchimba mchanga na kokoto za ujenzi.

Naye, Meneja wa Uwanja wa ndege wa Musoma, Mohammed Bakari, amesema kuwa uwanja huo utajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Beijing kutoka China na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.

Amefafanua kuwa Mkandarasi huyo tayari ameshawasilisha vifaa vyake katika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo, na kusisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mara.Hakuna kama Samia, View attachment 2029306
Nyerere haenziwi kwa kujenga viwanja vya ndege bali kwa kuheshimu
Urais ni taasisi Jomba,
Wewe tunajua kuwa ndiwe bi kidude mwenyewe unajisifia kwa majina bandia kwenye mitandao
 
BILIONI 35 KUJENGA UWANJA WA NDEGE MUSOMA KUMUENZI BABA WA TAIFA KWA VITENDO,​

3-25.jpg

Huu ni muonekano wa baadhi ya vifaa vya ujenzi vya mkandarasi Beijing kutoka nchini China ambavyo vinatarajiwa kutumika katika kazi za maboresho ya uwanja wa ndege wa Musoma sehemu aliyozaliwa muasisi wa Taifa hili,

Serikali ya Rais Samia Suluhu imesema inatarajia kutumia kiasi cha TZS 35BL ili kuboresha uwanja wa ndege wa Musoma,

Maboresho hayo ni pamoja na kuweka lami na kuongeza urefu wa uwanja huo ili kuruhusu ndege kubwa na ndogo kuweza kutua.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Musoma na pia kuchochea biashara ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo mkoani humo.

Ameongeza kuwa Uongozi wa Wilaya tayari umejipanga kwa kuupokea mradi huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkandarasi huyo kwa kumpatia eneo la kuchimba mchanga na kokoto za ujenzi.

Naye, Meneja wa Uwanja wa ndege wa Musoma, Mohammed Bakari, amesema kuwa uwanja huo utajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Beijing kutoka China na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.

Amefafanua kuwa Mkandarasi huyo tayari ameshawasilisha vifaa vyake katika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo, na kusisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mara.Hakuna kama Samia, View attachment 2029306
Huyo Mama tajiri sana

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Samia ametoa ni pesa ake mfukoni? hizi kodi za wananchi mbaya zaidi yeye hashiriki kulipa kodi mshahara wake haukatwi kodi. Ni dharau kubwa sn kwa wananchi
Tatizo lako ukisikia jina Samia unafananisha na jina la bibi yako kule kijijini!

Jina Samia linawakilisha taasisi ya urais.

Ndio maana Masoud alipoulizwa juu ya kuchora vikatuni vya Samia, alijibu kwamba yeye anachora urais na siyo mtu.

Bavicha mna vichwa vigumu sana.
 
Mkuu sami huo uwanja kaja kukamilisha tu mradi umeanza enzi za jiwe maan ata fidia watu wamelipwa wakat wake
Mtu kwao, hadi kufikia bajeti ya mwaka 2020/2021, hakukuwa na kitu kilichoendelea, kasome utekelezaji wa mpango wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi ukurasa wa 57 utaona mradi umeanza kufanyiwa kazi haswa mwezi Aprili mwaka huu na mama Samia ndio kamwaga pesa bilioni 35 cash ili mradi utekelezwe na kampuni kubwa kabisa ya ujenzi ya Beinjing Constructions ya China
 
Sasa hizo pesa Mwaka jana za fidia nani alitoa mkuu
 
Back
Top Bottom