BILIONI 35 KUJENGA UWANJA WA NDEGE MUSOMA KUMUENZI BABA WA TAIFA KWA VITENDO
Huu ni muonekano wa baadhi ya vifaa vya ujenzi vya mkandarasi Beijing kutoka nchini China ambavyo vinatarajiwa kutumika katika kazi za maboresho ya uwanja wa ndege wa Musoma sehemu aliyozaliwa muasisi wa Taifa hili,
Serikali ya Rais Samia Suluhu imesema inatarajia kutumia kiasi cha TZS 35BL ili kuboresha uwanja wa ndege wa Musoma,
Maboresho hayo ni pamoja na kuweka lami na kuongeza urefu wa uwanja huo ili kuruhusu ndege kubwa na ndogo kuweza kutua.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Musoma na pia kuchochea biashara ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo mkoani humo.
Ameongeza kuwa Uongozi wa Wilaya tayari umejipanga kwa kuupokea mradi huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkandarasi huyo kwa kumpatia eneo la kuchimba mchanga na kokoto za ujenzi.
Naye, Meneja wa Uwanja wa ndege wa Musoma, Mohammed Bakari, amesema kuwa uwanja huo utajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Beijing kutoka China na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.
Amefafanua kuwa Mkandarasi huyo tayari ameshawasilisha vifaa vyake katika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo, na kusisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mara.Hakuna kama Samia,