Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa

Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa

Tanzania kamwe hatutaendelea hivi karibuni ikiwa hatuna mwelekeo wala dira katika uongozi wa nchi. Kila rais ajaye anabuni mambo yake. Baya zaidi ni mambo haya ya kujitakia sifa. Uwanja wa ndege ni huduma/kitega uchumi, haujengwi kwa sababu ya kmuenzi mtu, yeyote. Sidhani kama kuna mtaala wowote uliofanywa juu uwanja huo utarudisha vipi pesa za watoa kodi. Inaelekea pesa za Watanzania zaamuliwa na mhumuko mmoja tu na mapenzi ya mtu! Nchi itaendelea vipi hivyo?
Natoa mfano wa Rwanda: kwa miaka 20 tu iliyopita Rwanda imepiga hatua kubwa sana ya kuigwa. Bila shaka sababu kuu ni kuwa kuna mwelekeo, dira na uongozi usobadilika badilika kama kinyonga.
Pili: Kwa nini kajiwanja kama haka kajengwe na Wachina? Jamani. Inadhi sana. Si muagize vyombo tu msivyonavyo? Mainjinia chungu nzima wapo. Walieni tu nusu ya mnavyowalipa Wachina watafanya kazi zaidi ya Wachina. Mbona Waafrika hatujiamini hivi?
 
Nenda kaishi RWANDA,,endelea kuishi kwa dadako
 
BILIONI 35 KUJENGA UWANJA WA NDEGE MUSOMA KUMUENZI BABA WA TAIFA KWA VITENDO​

3-25.jpg
Huu ni muonekano wa baadhi ya vifaa vya ujenzi vya mkandarasi Beijing kutoka nchini China ambavyo vinatarajiwa kutumika katika kazi za maboresho ya uwanja wa ndege wa Musoma sehemu aliyozaliwa muasisi wa Taifa hili.

Serikali ya Rais Samia Suluhu imesema inatarajia kutumia kiasi cha TZS 35BL ili kuboresha uwanja wa ndege wa Musoma,

Maboresho hayo ni pamoja na kuweka lami na kuongeza urefu wa uwanja huo ili kuruhusu ndege kubwa na ndogo kuweza kutua.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Musoma na pia kuchochea biashara ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo mkoani humo.

Ameongeza kuwa Uongozi wa Wilaya tayari umejipanga kwa kuupokea mradi huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkandarasi huyo kwa kumpatia eneo la kuchimba mchanga na kokoto za ujenzi.

Naye, Meneja wa Uwanja wa ndege wa Musoma, Mohammed Bakari, amesema kuwa uwanja huo utajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Beijing kutoka China na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.

Amefafanua kuwa Mkandarasi huyo tayari ameshawasilisha vifaa vyake katika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo, na kusisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mara.Hakuna kama Samia,
Kazi ya uwanja ni kumuenzi Mwl siyo kuboresha safari za anga
 
Tanzania na Samia,

1.Uchumi Juu,

2. Uwekezaji juu

3. Diplomasia juu

4. Amani & Upendo juu

5. Maendeleo juu

6. Demokrasia juu
 
Cheap!
Kumuenzi Mwalimu Nyerere kiuhalisia ni kumaliza Bwawa la Nyerere hilo lilikuwa ni wazo lake na kuhamia Dodoma, Nyerere alianzisha Mji Mkuu mpya wa Dodoma.

Yote mawili Bwawa la Nyerere na Dodoma Samia anayapiga vita, kama si kwa maneno basi kwa vitendo, angalau kulingana na matendo ya watendaji wake.
Mengine yote usanii tu.
Uko sahihi kabisa...

Nina wasiwasi huenda akarudi Kivukoni kabisa...

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Hivi ni ametoa au ameidhinisha???

Mnaposema ametoa, ametoa kutoka kwenye mwanzo vyake vya mapato au??
 
Cheap!
Kumuenzi Mwalimu Nyerere kiuhalisia ni kumaliza Bwawa la Nyerere hilo lilikuwa ni wazo lake na kuhamia Dodoma, Nyerere alianzisha Mji Mkuu mpya wa Dodoma.

Yote mawili Bwawa la Nyerere na Dodoma Samia anayapiga vita, kama si kwa maneno basi kwa vitendo, angalau kulingana na matendo ya watendaji wake.
Mengine yote usanii tu.
Sasa kuukamilisha bwawa si ni pesa? Tena ndefu
 
Tunazidi kufeli kila kukicha yaani Kuna shule hazina madarasa halafu tuna kazi ya kuenziana tu kweli Kama tz tumelogwa mchawi wetu yupo karibu Sana na sisi kuhakikisha hatufurukuti
Mkuu ujenzi wa madarasa umepamba moto sana kila shule unayopita kuna ujenzi.
 
Mh. Rais Samia, katika mengi yupo sahihi. Na kama nchi, endapo Samia angekuwa Rais tangu 2015, hakika nchi isingekuwa hapa ilipo leo.

Awamu ya 5, nchi ilikuwa inajengwa mdomoni, lakini kiuhalisia nchi ilikuwa ikizidi kuporomoka maeneno yote.

Samia, mahali pekee alipoboronga kabisa ni kumbambikia kesi Mbowe, na kuendelea kuwatesa makomandoo, ambao kwa uonevu mkubwa, utawala wa Magufuli, uliwatesa, kuwaonea, na huenda kuwaua baadhi.

Kama laiti Mama Samia angekaribiwa na hekima, japo kidogo sana, angeshauriana na DPP kuzifuta kesi hizi, na kuwalipa fidia vijana wetu makomandoo walioathirika afya zao kutokana na utumishi mwema, lakini kwa bahati mbaya, kwenye eneo hili, Samia ameamua kuendelea kujipakaza uchafu wa awamu ya 5 kwa kuendelea kuwatesa.

Makomandoo walistahili kuachiwa, na wahalifu wakubwa, mashetani wa kiwango cha ajabu, akina Kingai, Godluck, Mahita, Jumanne, Aziz, walistahili kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya utekaji, utesaji na mauaji.
 
Back
Top Bottom