Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa

Rais Samia atoa TZS 35BL Ujenzi wa Musoma Airport kumuenzi Baba wa Taifa

Katiba mpya na Bora ndiyo itaweza kuwa mkombozi wa kila kitu bila hiyo basi chozi la mnyonge litabaki kuwa Kama chozi la samaki kupotelea majini
Aliyetufanyia dhihaka ni huyu , mbona hakutuacha?
 
Attachments

  • VID-20211221-WA0013.mp4
    458.6 KB
Zanzibar haihitaji katiba mpya , inahitaji UHURU wake ulioporwa Na Tanganyika
Kitu ambacho hutaki kukiamini ni katiba mpya na Bora kuwa msaada kwa watu wote ila ukweli haubatilishwi kwa uongo Bali ukweli zaidi nikisema katiba mpya ni muhimu naona zaidi ya hapa tulipo,, kumbuka katiba ya wananchi ilipendekeza kuwa katika Tanzania na Zanzibar kuwe na serikali tatu maana yake hasa ni hiyo inamaana Visiwani kuwe na serikali yake Bara kuwe na serikali yake then tupate serikali ya tatu kwa ajili ya muungano,, je unaweza vipi kutenganisha Uhuru wa Zanzibar na Katiba mpya na Bora?
 
Aliyetufanyia dhihaka ni huyu , mbona hakutuacha?
Huyu alifanya yake kwa wakati wake na upeo wake hivyo ni wakati na zamu yetu kufanya yetu kwa wakati wetu ili wajukuu zetu wasituone vilaza kwa kuendeshwa na fikra na mitazamo ya marehemu
 
Tunazidi kufeli kila kukicha yaani Kuna shule hazina madarasa halafu tuna kazi ya kuenziana tu kweli Kama tz tumelogwa mchawi wetu yupo karibu Sana na sisi kuhakikisha hatufurukuti

Roho mbaya aikusaidii
 
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATOA TZS 35BL KUJENGA UWANJA WA "MUSOMA AIRPORT " ILI KUMUENZI HAYATI BABA WA TAIFA KWA VITENDO.​

3-25.jpg
Huu ni muonekano wa baadhi ya vifaa vya ujenzi vya mkandarasi Beijing kutoka nchini China ambavyo vinatarajiwa kutumika katika kazi za maboresho ya uwanja wa ndege wa Musoma karibu na Sehemu alikozaliwa muasisi wa Taifa hili Mwl Julius Kambarage Nyerere,

Serikali sikivu ya Rais Samia Suluhu Hassan imesema inatarajia kutumia kiasi cha TZS 35BL ili kuboresha uwanja wa ndege wa Musoma uliotelekezwa na awanu zote tangu Uhuru,

Maboresho hayo ni pamoja na kuweka lami na kuongeza urefu wa uwanja huo ili kuruhusu ndege kubwa na ndogo kuweza kutua mkoa wa Mara,,Uwanja huu pia utahudumia na maeneo ya jirani kama Simiyu na Mwanza,

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Khalfani Haule, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utarahisisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Musoma|Mara na pia kuchochea biashara ya utalii kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo ipo mkoani humo kwani kabla Watalii wengi walishuka uwanja wa KIA,

Ameongeza kuwa Uongozi wa Wilaya tayari umejipanga kwa kuupokea mradi huo na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mkandarasi huyo kwa kumpatia eneo la kuchimba mchanga na kokoto za ujenzi.

Naye, Meneja wa Uwanja wa ndege wa Musoma, Mohammed Bakari, amesema kuwa uwanja huo utajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Beijing kutoka China na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022.

Amefafanua kuwa Mkandarasi huyo tayari ameshawasilisha vifaa vyake katika eneo la mradi kwa ajili ya kuanza rasmi ujenzi huo, na kusisitiza kuwa ujenzi wa uwanja huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Mara.Hakika hakuna kama Rais Samia Suluhu Hassan,
Hongera Rais Samia kwa jicho lako kufika huku. Mwalimu Nyerere anastahili kuheshimishwa na wewe umeliona hilo.
 
Huyu alifanya yake kwa wakati wake na upeo wake hivyo ni wakati na zamu yetu kufanya yetu kwa wakati wetu ili wajukuu zetu wasituone vilaza kwa kuendeshwa na fikra na mitazamo ya marehemu
Mzimu Wake CCM bado unatuendesha mbio
 
Mzimu Wake CCM bado unatuendesha mbio
Hahahahaaa Mimi sipo aisee huo mzimu wa marehemu Wala haunijui na hautakaa unijue ndiyo maana nakuwa kinyume na wafuasi wa CCM maana najua wanarumia akili ya marehemu mpaka leo
 
Kitu ambacho hutaki kukiamini ni katiba mpya na Bora kuwa msaada kwa watu wote ila ukweli haubatilishwi kwa uongo Bali ukweli zaidi nikisema katiba mpya ni muhimu naona zaidi ya hapa tulipo,, kumbuka katiba ya wananchi ilipendekeza kuwa katika Tanzania na Zanzibar kuwe na serikali tatu maana yake hasa ni hiyo inamaana Visiwani kuwe na serikali yake Bara kuwe na serikali yake then tupate serikali ya tatu kwa ajili ya muungano,, je unaweza vipi kutenganisha Uhuru wa Zanzibar na Katiba mpya na Bora?

Tatizo Huo Si muungano ni uvamizi uliopewa Jina la muungano , huwezi haramu kuifanya halali
 
Tatizo Huo Si muungano ni uvamizi uliopewa Jina la muungano , huwezi haramu kuifanya halali
Unafikiri ni njia gani inafaa kutumia kutoka kwenye uvamizi huo bila kupitia kivuli Cha katiba mpya na Bora ? Maana kwa nguvu ya umma ni ngumu kwasababu usaliti upo mkubwa Sana tunasalitiana sisi kwa sisi
 
Cheap!
Kumuenzi Mwalimu Nyerere kiuhalisia ni kumaliza Bwawa la Nyerere hilo lilikuwa ni wazo lake na kuhamia Dodoma, Nyerere alianzisha Mji Mkuu mpya wa Dodoma.

Yote mawili Bwawa la Nyerere na Dodoma Samia anayapiga vita, kama si kwa maneno basi kwa vitendo, angalau kulingana na matendo ya watendaji wake.
Mengine yote usanii tu.
Sukuma gang mnapata tabu sana
 
Samia ametoa ni pesa ake mfukoni? hizi kodi za wananchi mbaya zaidi yeye hashiriki kulipa kodi mshahara wake haukatwi kodi. Ni dharau kubwa sn kwa wananchi
Hii lugha ya kijinga kuliko maelezo inalidharirisha mpk bunge in a way. Huu ujinga ukome sasa enough is enough jamani.
 
Cheap!
Kumuenzi Mwalimu Nyerere kiuhalisia ni kumaliza Bwawa la Nyerere hilo lilikuwa ni wazo lake na kuhamia Dodoma, Nyerere alianzisha Mji Mkuu mpya wa Dodoma.

Yote mawili Bwawa la Nyerere na Dodoma Samia anayapiga vita, kama si kwa maneno basi kwa vitendo, angalau kulingana na matendo ya watendaji wake.
Mengine yote usanii tu.
Usidhani kujenga umeme wa Stiglers Gorge watangulizi wa Magufuli walishindwa, la hasha. Nyerere pamoja na waliomfuata walishauriwa na wakashaurika kuwa madhara ya kujenga DAM ndani ya pori la Selous ni makubwa kuliko faida zake licha ya kwamba kuna nia nyingine ya kuzalisha Megawati 2,100.

Kuhusu kuhamia Dodoma nako sababu zake zilipitwa na wakati ambapo baada ya kuisha cold war ya Warsaw pact/NATO hakukuwa tena na justification. Kuhamia Dodoma ni misusue ya kodi za wananchi tu
 
Unafikiri ni njia gani inafaa kutumia kutoka kwenye uvamizi huo bila kupitia kivuli Cha katiba mpya na Bora ? Maana kwa nguvu ya umma ni ngumu kwasababu usaliti upo mkubwa Sana tunasalitiana sisi kwa sisi

Kwani hiyo katiba mpya Kuna hakika gani ya kufuatwa? CCM wanapata kiburi kwa kuwa Kuna mkono wa Waingereza nyuma , basi.

Nyerere alishapinduliwa Na wanajeshi Na waliomrudisha madarakani ni waingereza Na kuanzia wakati Huo nchi iko rehani. Na kazi kubwa aliyopewa Nyerere ni kuivamia Zanzibar Na kuidhibiti. La muhimu kufanya ni kwa waTanganyika kudai nchi yao Kama walivyofanya G50
 
Team JF,

MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR 2022.

#TUENDELEE KUMUUNGA MKONO RAIS WETU,
 
Happy Boxing Day kwa hisani ya Mhe Samia Suluhu Hassan
 
Miradi yote iliyoachwa na Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli Rais Samia Suluhu Hassan anaitekeleza kwa 100%

Sihiyo tu tayari mingine mipya inaendelea na Ujenzi,

Tunawajibu wa kumwombea Mama huyu,
 
Back
Top Bottom