Rais Samia atoa wastani wa madarasa manne na madawati 120 katika kila shule ya Sekondari nchi nzima

Kwani asingefanya mngemlaumu nani?



Anawezaje haya yote huyu mama?

SGR TZS 10.2T ni Yeye,
SG TZS 6.55T ni Yeye
Madarasa mapya manne kila sekondari nchi nzima,
Madawati 120 kila sekondari nchi nzima
Acheni ujuha nyie watu
Raisi hatoi pesa mfukoni mwake! Anachokifanya yeye ni kusimamia mgawo tu. Wala siyo HISANI au UPENDELEO. wewe na mm na bibi yako kijijini tutakuja kulipa.
Ni amma kwa kutojua kwako au kutanguliza siasa kuliko nchi kuwadanganya watu kwamba raisi SSH katoa hiki na hiki.
Mmezoeshwa kuongea UONGO na lile fedhuli LENU lilokufa kwa CORONA
MAJUHA WAKUBWA
 
Mikopo ni aina nyingine ya ukoloni ndio maana baba yenu mwendazake alikua anajitahidi kuikwepa, kwanza kwanini wanakopa wakati walisema tumekubaliana tozo na Kodi kwenye miamala na mafuta pesa zake zitatumika kujenga hiyo miundombinu waliyoitaja
Maskini ukikwepa mikopo utakufa,huo ujanja hakuwa nao
 
We kweli unaostahili pole..

Kwako wewe afya haijengi uchumi,umeme haujengi uchumi,utalii haujengi uchumi na uwekezaji kwenye sekta ya elimu haujengi uchumi.

Kujenga uchumi ni kujenga madaraja,umeme tuu 😄😄😄😄😄
 
Kwanini tunaenda kukopa wakati tayari tulishaweka mipango ya ndani kuwezesha hizo sekta ie tozo na Kodi kwenye miamala na mafuta tuliambiwa ni kwa ajili ya mambo yaleyale yanayotajwa kwenye huo mpango wa mkopo wa IMF huoni kuna harufu ya ufisadi hapo
 
Huyu rais ni mchapakazi, huyu ndiye tuliyemhitaji.
 
Kwanini tunaenda kukopa wakati tayari tulishaweka mipango ya ndani kuwezesha hizo sekta ie tozo na Kodi kwenye miamala na mafuta tuliambiwa ni kwa ajili ya mambo yaleyale yanayotajwa kwenye huo mpango wa mkopo wa IMF huoni kuna harufu ya ufisadi hapo
Mipango kama imevurugwa na janga utaendelea na kusubiria mipango?
 
Habari njema sana hii.
 
Kazi nzuri sana.
 
Huyu naona anaelekea kuwateka wananchi, naona kila dalili za kufanya vizuri tofauti na tulivyomchukulia katika mtazamo hasi! Taratibu anaeleweka.
Wataka atuteke mara ngapi?Na kila mwananchi ukimsomea hizi habari,anafurahi.
 
Kumbe kila Shule madawati 120,
Kila shule madarasa 4
Samia analeta raha sana huyu mama,
Mimi nimeshuhudia marais wanne ila huyu ni watofauti sana,
Huyu Rais,ni wa kipekee,kila mwananchi akisikia,anahutubia,anajisogeza kwenye TV,asikize mapya.
 
Acha utoto! Hii kauli ya ....NCHI NZIMA tulishaizoea na ina ukakasi. Mlitwambia kila kijiji kitapewa 15M mwishoni mkatuchinjia baharini. Hatuna imani na ahadi zenu tena mjue!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…