Rais Samia atua Namibia kumzika Hayati Dkt. Geingob

Kazi tunayo aisee.

Si alikua Ethiopia juzi tu hapo na tena ni baada ya kutoka Vatican, Norway, na kwenye mazishi ya Lowasa.

Ofisini anakaa saa ngapi huyu??
Unataka awe anakaa ofisini kama zuzu?, safari zote huwa za kikazi, hii ya leo ni ya mazishi.
 
Hivi hizi safari huwa anapanga yeye au anapangiwa watu wapige posho
Safari ya mazishi imepangwa na kifo mkuu.

Marais wa nje wamekuja kumzika rais wetu alipofariki.

Ni wajibu wetu kumtuma rais wetu aende kuzika marais wa nje wa nchi zenye uhusiano mzuri nasi.

Ndiyo diplomasia ya kimataifa inavyokwenda hivyo.

Hii kanuni ya diplomasia inaitwa "reciprocity".

Mnaweza kumlaumu Samia kwenye safari nyingine, lakini si kwa safari ya kwenda kumzika rais wa Namibia.

Namibia na Tanzania ni nchi zenye uhusiano mrefu sana.

Tumewa host wakimbizi wa Namibia wamekaa Tanzania mpaka wamepata uhuru.

Sasa tuje kuwatupa mkono leo kwenye msiba wa rais wao?
 
Kazi tunayo aisee.

Si alikua Ethiopia juzi tu hapo na tena ni baada ya kutoka Vatican, Norway, na kwenye mazishi ya Lowasa.

Ofisini anakaa saa ngapi huyu??
Yule Mama kasha changanyikiwa,anajifariji na safari tu!
 
Dah
Anyways Mungu ampokee mja wake
 
Samia, she is really stateswoman. Pride of Tanzania and Africa.
 
Hivi huo mdudu unatumia fuel kidogo kuliko Gulf stream
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…