Rais Samia Atuma Salamu Nzito za Pongezi kwa Rais wa Afrika kusini kwa kuchaguliwa kwake Awamu ya pili.

Rais Samia Atuma Salamu Nzito za Pongezi kwa Rais wa Afrika kusini kwa kuchaguliwa kwake Awamu ya pili.

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan ametuma salamu nzito za pongezi kwa Mheshimiwa Cyril Ramaphosa ,kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindoo kwa muhula wa pili kama Rais wa Taifa hilo.

Salamu hizo zimetolewa na Rais wetu kupitia mtandao wa Twitter,ambapo amempongeza sana kwa imani kubwa aliyopewa ya kuendelea kuliongoza Taifa la Afrika kusini,lakini pia Rais wetu ameahidi kuendelea kushirikiana naye na Taifa la Afrika kusini na kuendeleza Historia yetu ya kindugu na ya muda mrefu.

Mheshimiwa Ramaphosa ameshinda Urais huo baada ya kupata kura karibu 283 na kumshinda mgombea wa chama cha EFF kinachoongozwa na Mhessimiwa Julius Malema aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa vijana wa chama cha ANC kabla ya kutimuliwa kwenye chama hicho.Na kuunda chama chake cha Economic Freedom Fighters. Ambapo kwa sasa chama chake kilipata kura 9% na kuzidiwa na chama cha Mheshimiwa Zuma kilichoanzishwa miezi michache tu iliyopita kilichopata 15%.

Lakini pia uchaguzi huu umeshuhudia ANC ikiporomoka vibaya sana katika Historia ya uchaguzi wa Taifa hilo na kushindwa kufikisha 50% ya kura. Jambo lililopelekea ANC kufanya mazungumzo na chama cha DA kilichopata 22% ya kura zote.

Naamini ANC na viongozi wake watakuja haraka sana Tanzania kujifunza kwa CCM naamna ya kurejesha imani ya wapiga kura kilio wapoteza na waliokinyima kura. Kikubwa ANC inatakiwa ijifunze kwa CCM kuhakikisha kuwa kinakuwa karibu ya wananchi wake, kuwasikiliza kero zao na kuwapatia majibu,kuwa na sera zenye kuleta matumaini kwa watu hasa kundi la vijana ambalo ndio kundi kubwa.

Kwa kuhakikisha kuwa kundi hili linapewa kipaombele ya kisera,kibajeti na kifursa,kama ambavyo CCM imekuwa ikifanya hapa Nchini kwa kutoa kipaombele kwa vijana,kwa kuwapatia ajira,mikopo pamoja na kuwawezesha kwa namna tofauti tofauti. ndio sababu vijana wameendelea kuiamini na kuipigia CCM kura kila uchaguzi.

Lakini pia ni lazima ANC ni lazima ijifunze kwa CCM kuwa na sera zinazoendana na mahitaji ya wakati na zenye kugusa kila kundi na maisha yao,kutumia rasilimali zake zote kujenga miundombinu na miradi itakayotoa fursa za ajira kwa vijana ,pamoja na kuwajengea matumaini hai wananchi wake.ambapo mtu akiamka awe na matumaini ya kupata walau milo mitatu kwa siku, uhakika wa kupata matibabu mtu akiugua,uhakika wa kupata Elimu kijana akifaulu,uhakika wa kupata ajira akimaliza chuo kikuu au kujiajiri katika mazingira salama na rafiki,uhakika wa usalama kwa shughuli zake,uhakika wa watu hasa vijana kujiona fahari kuzaliwa Afrika kusini kama ilivyo kwa watanzania kufurahia kuzaliwa hapa Nchini.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Hata urudie mara ngapi kuandika hii sentensi tambua yafuatayo.
1. Hakuna uteuzi utakaoambulia kipindi cha mama Samia.
2. Rais Samia atakuwa Rais mstaafu punde baada ya uchaguzi wa 2025.
Moja ni kuwa mimi sijasema kuwa naandika na nipo hapa jukwaani kwa ajili ya kutafuta uteuzi.

Pili ni kuwa Watanzania kwa furaha, bashasha na matumaini makubwa sana vifuani mwetu tutaendelea kudunda na kutamba na Rais Samia mpaka 2030.ambapo hapo ndio kituo cha kupumzikia na kuangalia sasa tufanye nini .ila kwa sasa hakuna mjadala juu ya kugombea kwa Rais Samia maana ni chaguo letu ni Yeye ambaye ni yeye tunayemuamini kwa sasa.
 
Uandishi wako unanipa tabu. Badala ya kuelezea taarifa kikamilifu unajaza maneno mengi mengine yasiyo na tija.
Acha uvivu na papala zako hapa.kipi ambacho hujaelewa hapo .taarifa ni kuwa Rais Samia kampongeza Mheshimiwa Ramaphosa kwa kuchaguliwa kwake Awamu ya pili.na na kuahidi kuendelea kushirikiana naye kuendeleza undugu na ushirikiano wetu wa kihistoria.
 
Moja ni kuwa mimi sijasema kuwa naandika na nipo hapa jukwaani kwa ajili ya kutafuta uteuzi.

Pili ni kuwa Watanzania kwa furaha, bashasha na matumaini makubwa sana vifuani mwetu tutaendelea kudunda na kutamba na Rais Samia mpaka 2030.ambapo hapo ndio kituo cha kupumzikia na kuangalia sasa tufanye nini .ila kwa sasa hakuna mjadala juu ya kugombea kwa Rais Samia maana ni chaguo letu ni Yeye ambaye ni yeye tunayemuamini kwa sasa.
1. Moja ni kwa kuwa unajipendekeza sana, hivyo hata usipoandika kuwa unahitaji uteuzi ila Kila mwenye akili timamu akiona andiko lako atajua kuwa unajipendekeza ili uteuliwe.

2. Juu ya Rais Samia kuwa Rais mstaafu kuanzia 2025 November (labda aahirishe uchaguzi ili aendelee kuwa Rais), subiri uone hiyo 2025.
 
Kwa miaka niliyokaa JF nimepata uzoefu kiasi kwamba nikiona tu heading ninajua ni mtu fulani ndio mwenye thread hata bila kuangalia jina.Nikionaga tu title ina samia najua kuna posibilities ni chawa andamizi mwashambwa
 
1. Moja ni kwa kuwa unajipendekeza sana, hivyo hata usipoandika kuwa unahitaji uteuzi ila Kila mwenye akili timamu akiona andiko lako atajua kuwa unajipendekeza ili uteuliwe.

2. Juu ya Rais Samia kuwa Rais mstaafu kuanzia 2025 November (labda aahirishe uchaguzi ili aendelee kuwa Rais), subiri uone hiyo 2025.
Moja, mimi sijipendekezi bali huandika UKWELI tu bila kujali ukweli huo ni mchungu Kiasi gani kwa watu aina yako wasiopenda kusikia ukweli.

Pili ,hakuna mwenye ubavu wala uwezo wala nguvu wala ushawishi wa kuweza kushindana na Rais Samia katika sanduku la kura .mtu huyo hayupo kabisa na wala hajazaliwa kutoka huko upinzani.
 
Naamini ANC na viongozi wake watakuja haraka sana Tanzania kujifunza kwa CCM naamna ya kurejesha imani ya wapiga kura kilio wapoteza na waliokinyima kura. Kikubwa ANC inatakiwa ijifunze kwa CCM kuhakikisha kuwa kinakuwa karibu ya wananchi wake, kuwasikiliza kero zao na kuwapatia majibu,kuwa na sera zenye kuleta matumaini kwa watu hasa kundi la vijana ambalo ndio kundi kubwa.
Wajifunze nini.....?
 
Moja ni kuwa mimi sijasema kuwa naandika na nipo hapa jukwaani kwa ajili ya kutafuta uteuzi.

Pili ni kuwa Watanzania kwa furaha, bashasha na matumaini makubwa sana vifuani mwetu tutaendelea kudunda na kutamba na Rais Samia mpaka 2030.ambapo hapo ndio kituo cha kupumzikia na kuangalia sasa tufanye nini .ila kwa sasa hakuna mjadala juu ya kugombea kwa Rais Samia maana ni chaguo letu ni Yeye ambaye ni yeye tunayemuamini kwa sasa.
Ongezea tumetokwa na machozi ya furaha baada ya kusikia salam nzito za Daktari samiah suluhu Hassan mh .Rais
 
Lucas mbona umenikimbia kule kwenye uzi!? Nilipie 500k niwe platinum member...!🤸
Sijakukimbia lazizi wangu ila nilikuwa naangalia namna mipango ifanyike ya sherehe ya kukupatia U platinum humu jukwaani kusudi siku hiyo shughuli zote za JF zisimamishwe. na wewe uwe ndio Mgeni Rasmi humu na kutoa neno mpaka watu wabaki wanabubujikwa na machozi utafikiri wameingiwa na mchanga machoni.
 
Dr Restart umemuelewa Lucas?
 
Back
Top Bottom