Rais Samia Atuma Salamu Nzito za Pongezi kwa Rais wa Afrika kusini kwa kuchaguliwa kwake Awamu ya pili.

Rais Samia Atuma Salamu Nzito za Pongezi kwa Rais wa Afrika kusini kwa kuchaguliwa kwake Awamu ya pili.

Ona haya mapumbavu mengine.Usikute limwashambwa na lenyewe limo humu linacheza chikichi chikichi eeh chikichi chikichi eeh
20240615_144805.jpg

Mimi siyo chawa bali ni msema kweli.
Nimesheshangazwa mno ujinga unauita ukweli hizo salamu alizozituma unazoziita nzito zina kila ngapi ndio maana nakuita mjinga
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan ametuma salamu nzito za pongezi kwa Mheshimiwa Cyril Ramaphosa ,kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindoo kwa muhula wa pili kama Rais wa Taifa hilo.

Salamu hizo zimetolewa na Rais wetu kupitia mtandao wa Twitter,ambapo amempongeza sana kwa imani kubwa aliyopewa ya kuendelea kuliongoza Taifa la Afrika kusini,lakini pia Rais wetu ameahidi kuendelea kushirikiana naye na Taifa la Afrika kusini na kuendeleza Historia yetu ya kindugu na ya muda mrefu.

Mheshimiwa Ramaphosa ameshinda Urais huo baada ya kupata kura karibu 283 na kumshinda mgombea wa chama cha EFF kinachoongozwa na Mhessimiwa Julius Malema aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa vijana wa chama cha ANC kabla ya kutimuliwa kwenye chama hicho.Na kuunda chama chake cha Economic Freedom Fighters. Ambapo kwa sasa chama chake kilipata kura 9% na kuzidiwa na chama cha Mheshimiwa Zuma kilichoanzishwa miezi michache tu iliyopita kilichopata 15%.

Lakini pia uchaguzi huu umeshuhudia ANC ikiporomoka vibaya sana katika Historia ya uchaguzi wa Taifa hilo na kushindwa kufikisha 50% ya kura. Jambo lililopelekea ANC kufanya mazungumzo na chama cha DA kilichopata 22% ya kura zote.

Naamini ANC na viongozi wake watakuja haraka sana Tanzania kujifunza kwa CCM naamna ya kurejesha imani ya wapiga kura kilio wapoteza na waliokinyima kura. Kikubwa ANC inatakiwa ijifunze kwa CCM kuhakikisha kuwa kinakuwa karibu ya wananchi wake, kuwasikiliza kero zao na kuwapatia majibu,kuwa na sera zenye kuleta matumaini kwa watu hasa kundi la vijana ambalo ndio kundi kubwa.

Kwa kuhakikisha kuwa kundi hili linapewa kipaombele ya kisera,kibajeti na kifursa,kama ambavyo CCM imekuwa ikifanya hapa Nchini kwa kutoa kipaombele kwa vijana,kwa kuwapatia ajira,mikopo pamoja na kuwawezesha kwa namna tofauti tofauti. ndio sababu vijana wameendelea kuiamini na kuipigia CCM kura kila uchaguzi.

Lakini pia ni lazima ANC ni lazima ijifunze kwa CCM kuwa na sera zinazoendana na mahitaji ya wakati na zenye kugusa kila kundi na maisha yao,kutumia rasilimali zake zote kujenga miundombinu na miradi itakayotoa fursa za ajira kwa vijana ,pamoja na kuwajengea matumaini hai wananchi wake.ambapo mtu akiamka awe na matumaini ya kupata walau milo mitatu kwa siku, uhakika wa kupata matibabu mtu akiugua,uhakika wa kupata Elimu kijana akifaulu,uhakika wa kupata ajira akimaliza chuo kikuu au kujiajiri katika mazingira salama na rafiki,uhakika wa usalama kwa shughuli zake,uhakika wa watu hasa vijana kujiona fahari kuzaliwa Afrika kusini kama ilivyo kwa watanzania kufurahia kuzaliwa hapa Nchini.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Rubbish
 
Ungalijua DA ni chama cha akinanani usingesifia hili. Unaingia katika kuiongoza nchi na wale watesi wenu wa hapo awali halafu unajidai kuiongoza nchi kwa kipindi kingine.
 
Ungalijua DA ni chama cha akinanani usingesifia hili. Unaingia katika kuiongoza nchi na wale watesi wenu wa hapo awali halafu unajidai kuiongoza nchi kwa kipindi kingine.
Embu niambie kwanini wananchi wamechagua na kukipatia kura chama cha Democratic Alliance? Kwamba wao hawaifahamu historia ya Taifa lao? Kwanini wasikipe EFF cha Malema au kile cha Zuma cha wapigania uhuru? Tambua kuwa wananchi wamevuka mstari wa ubaguzi na kuangalia chama chenye sera na ajenda zenye kugusa maisha yao ya kila siku. Kuna faida gani ya kung'ang'ania mtu anayekuumiza ,kukutesa,kukunyonya na kukuangamiza? Muache kidogo na kukaa naye mbali kidogo ili ajuwe kuwa hufurahii matendo yake .akijisahihisha na kujirekebisha utamrudia baadaye.
 
Acha uvivu na papala zako hapa.kioi ambacho hujaelewa hapo .taarifa ni kuwa Rais Samia kampongeza Mheshimiwa Ramaphosa kwa kuchaguliwa kwake Awamu ya pili.na na kuahidi kuendelea kushirikiana naye kuendeleza undugu na ushirikiano wetu wa kihistoria.
Safi sana. Embu angalia sasa ulivyoandika kwa ufupi na fasaha.

Ndiyo hivyo ulitakiwa kuandika.
 
Embu niambie kwanini wananchi wamechagua na kukipatia kura chama cha Democratic Alliance? Kwamba wao hawaifahamu historia ya Taifa lao? Kwanini wasikipe EFF cha Malema au kile cha Zuma cha wapigania uhuru? Tambua kuwa wananchi wamevuka mstari wa ubaguzi na kuangalia chama chenye sera na ajenda zenye kugusa maisha yao ya kila siku. Kuna faida gani ya kung'ang'ania mtu anayekuumiza ,kukutesa,kukunyonya na kukuangamiza? Muache kidogo na kukaa naye mbali kidogo ili ajuwe kuwa hufurahii matendo yake .akijisahihisha na kujirekebisha utamrudia baadaye.
Umenena vyema. Hata hapa Peru tujiulize kama kunavfaida gani kung'ang'snia hawa watesi wetu? Muda utaongea.
 
Back
Top Bottom