Rais Samia Atunukiwa Tuzo Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya

Rais Samia Atunukiwa Tuzo Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunikuwa tuzo ya Kutambua mchango wake kwenye mapambano dhidi ya dawa za Kulevya nchini.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwake na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyeiwasilisha kwa niaba ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Rais Samia amepewa tuzo hiyo katika maadhimisho ya kitaifa ya kupiga vita matumizi na biashara ya dawa hizo duniani ambayo kitaifa yamefanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo Jumapili Juni 25, 2023.
Tz ni shamba la maajabu na maigizo. Duniani kote hayapo
 
Makonda alikuwa anawabambika watu kesi A madawa ya kulevya halafu anapewa magari ya watu jambazi yule.
 
akisafishwa na kuondolewa international sanctions aliyowekewa, Paul Christian Makonda Bashite anaweza kua kiongozi mzuri tu. Kumuingiza serikalini akiwa na kikwazo kimataifa ni kuikaribisha Jumuiya ya kimataifa kuanza kuchunguza serikali yako inafanya nini na bwana huyu.
 
Back
Top Bottom