Yesu Kristo hana kabila wala utaifa mara zote makabila tunarithishwa na baba zetu hivyo Yesu Kristo in reality sio Myahudi kwa vile alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ambaye hana kabila ni Neno lilolonenwa likafanyika mwili kama ilivyoandikwa kwenye Yohana 1:14 ila kuitwa kwake Simba wa kabila la Yuda ni sehemu ya kutimiza unabii wa kuja kwake kwa kwanza ambapo alionesha kuwa ni Mfalme wa Wayahudi ambao walimkataa na kumwangika msalabani kama ilivyoandikwa kwenye msalaba.Hivyo Yesu alisema "Mimi nasema nao kwa mifano,ili wakisikia wasielewe wakitazama wasione bali ninyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu ila wengine hawakujaliwa.Hivyo Simba wa kabila la Yuda ni mfano wa kuonesha ufalme Wake kwa Israel kwa vile katika mpangilio wa majukumu ya waliyopewa wana wa Israel kulingana na makabila 12 Yuda waliwakilisha Simba na ndio walikuwa vinara wa makabila matatu ambayo yalijipanga kwa kulinda pande nne za dunia ambayo Yuda alisimama mashariki kulinda sanduku la agano mengine yalisimama upande wa magharibi,kaskazini na kusini kwa idadi ya makabila matatu matatu.Hivyo makabila hayo yaliwakilisha wenye uhai wanne yaani Simba,Ndama,Uso wa mwanadamu na Tai arukaye.