Rais Samia atuombe msamaha Wakristo, Simba wa Yuda kwetu ni Yesu Kristo peke yake

Hakuna anayekataa kwamba Rais Samia anaponyesha majeraha yaliyoletwa na awamu zilizopita hususani ya tano lakini Simba wa Yuda si jina la kumfananisha na mwanadamu.
Kwani Yesu alikuwa Simba kiukweli au ni maneno tu?
 
Mmemchokoza mama kwa kusema ni dhaifu, sasa na yeye ameamua kufungulia mbwa. Hakika tutayasikia na kuyaona mengi.
 
Kwani Yesu alikuwa ni Simba kweli ama ni maneno tu ya waimba kwaya na mapambio?
 
Ila ujumbe wake umefika.
.................................................

Ni kweli tuna heshima ya uoga ila asisahau kuwa uoga huo umelelewa na kukuzwa mfumo ambao upo mpaka sasa kwa hiyo tatizo siyo uoga wetu ila mfumo ndiyo unaosababisha tuwe waoga.

Tuna heshima ya uoga ili viongozi wetu waweze kupitisha kila wanachopanga.
 
Sasa Mungu anakuwaje Simba?
Au mwana wa mungu anakuwaje Simba?
Ninyi, si huwa mnasema mnyezi mungu wenu hashindwi chochote, sasa inakuwaje tena ashindwe kujiwekea hali au umbile la simba [emoji848][emoji1787]

Mwisho wa siku Simba anayetajwa hapo ni katika methali za Biblia, na huwezi kuelewa mpaka Roho Mtakatifu akufundishe na kukuongoza [emoji16]
 
Kweli kumwita Hayati Magufuli Simba wa Yuda si sawa kabisa. Ni dharau kubwa sana kwa sisi waumini wa dini ya Kikristo.

Maana kwetu sisi Yesu Kristo ndiye Simba wa Yuda.

Rais kweli hapa si sawa kabisa.
Wakristo vita vya Yesu huwa tunamwachia Yeye Aliye Simba wa Kabila la Yuda.

Unakumbuka Lugola alimwiita JPM Yesu na wala JPM mwenyewe alipokea sifa hizo bila kumkemea Lugola?

Wakristo hatuwezi kumpambania Yesu yeye ndiye atupambaniaye.

Asimbe radhi asubiri majibu
 
Kawawa aliitwa Simba wa Yuda, alikuwa na utukufu upi wenye kufanana na Yesu?. Mbona jina lake lilidumu na hakuna hata mmoja aliyeleta nongwa za kujifanya anamjua sana Yesu?.
We mvaa kobazi mwenye user name ya Phillipo Kawawa aliitwa simba wa vita
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…