Rais Samia aunda Wizara Mpya na kufanya Mabadiliko ya kimuundo baadhi ya Wizara. Amteua Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri

Sasa Kitila chapa kazi kwa bidii na maarifa yako yote.

Rais amekuamini basi nawe uaminike.
 
Kuna watu huwa nawaeleza hili jambo hawaelewi,huwezi kutegemea wageni washike njia kuu za uchumi at the same time utegemee watu wako waondoke kwenye umasikini.
Imagine huko kwenye madini gas na kwingine,kama watanzania ndio wangekuwa wanashiriki fedha zote zingebaki ndani.
 
Naona mama anazidi kupotea. Huu uteuzi wa Mkumbo ameufanya kwa pressure tu. Tusitegemee matokeo chanya yoyote
 
Azimio la bandari Kitila Mkumbo ndio alikuwa wa Kwanza kuongea bungeni na aliitumia vizuri hiyo nafasi
Katika kikao cha ndani cha CCM alikuwa ni mpingaji mkuu wa suala la bandari, Alipewa shule nzito ya suala zima na Hamza Johari aliposimama na akabadilika na kuwa muungaji mkono mkubwa.
 
Si chochote, si lolote!
 
Prof mkumbo siku ya kupitisha mkataba bungeni, akivyopiga debee, haya huku nje kila leo kusifia, kumbe alikua anataka ulajiii.

Woiiiiiiiih, ni tengua na teuaa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kaziii ipoo
Ana kampuni zake pia za Clearing uyo...
 
Naomba mwenye Majibu ya swali langu anisaidie, maana kwa akili yangu ndogo nimeshindwa kupata majibu, nina maanisha sababu hasa zilizomsukuma Rais kumteua huyu jamaa kwenye Uwaziri.

Angalizo: Sitaki atukanwe au adhalilishwe, nimeuliza hili kwa Maslahi Mapana ya Taifa

Naomba kuwasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…