Rais Samia aunda Wizara Mpya na kufanya Mabadiliko ya kimuundo baadhi ya Wizara. Amteua Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri

Rais Samia aunda Wizara Mpya na kufanya Mabadiliko ya kimuundo baadhi ya Wizara. Amteua Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri

Sasa Kitila chapa kazi kwa bidii na maarifa yako yote.

Rais amekuamini basi nawe uaminike.
 
Nchi isiyowekeza kwenye R&D, itaendelea kuburuzwa hadi kiama...

Nchi inayotegemea siasa na wanasiasa kuleta mapinduzi ya kiuchumi au maendeleo ya kiuchumi, itaendelea kuburuzwa hadi kiama...

Nchi inayotegemea wajenzi wa nchi wawe ni wageni na sio wazawa, itaendelea kuburuzwa hadi kiama...
Kuna watu huwa nawaeleza hili jambo hawaelewi,huwezi kutegemea wageni washike njia kuu za uchumi at the same time utegemee watu wako waondoke kwenye umasikini.
Imagine huko kwenye madini gas na kwingine,kama watanzania ndio wangekuwa wanashiriki fedha zote zingebaki ndani.
 
Naona mama anazidi kupotea. Huu uteuzi wa Mkumbo ameufanya kwa pressure tu. Tusitegemee matokeo chanya yoyote
 
Azimio la bandari Kitila Mkumbo ndio alikuwa wa Kwanza kuongea bungeni na aliitumia vizuri hiyo nafasi
Katika kikao cha ndani cha CCM alikuwa ni mpingaji mkuu wa suala la bandari, Alipewa shule nzito ya suala zima na Hamza Johari aliposimama na akabadilika na kuwa muungaji mkono mkubwa.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Kitila Mkumbo kuwa Waziri. Aidha amefanya mabadiliko madogo ya miundo katika baadhi ya Wizara.

---
PROF. KITILA MKUMBO AWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI

Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na kumteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mbunge wa Jimbo la Ubungo) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji

Ni baada ya kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala a uwekezaji Ofisi ya Rais
-

DKT. MWIGULU NCHEMBA AWA WAZIRI WA FEDHA

Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Wizara ya Fedha na kumteua Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Fedha

Hapo awali alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango
-

DKT. ASHATU KIJAJI AWA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA

Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Wizara ya Viwanda na kumteua Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Wizara hiyo

Hapo awali alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara


Si View attachment 2679459
Si chochote, si lolote!
 
Prof mkumbo siku ya kupitisha mkataba bungeni, akivyopiga debee, haya huku nje kila leo kusifia, kumbe alikua anataka ulajiii.

Woiiiiiiiih, ni tengua na teuaa. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kaziii ipoo
Ana kampuni zake pia za Clearing uyo...
 
Naomba mwenye Majibu ya swali langu anisaidie, maana kwa akili yangu ndogo nimeshindwa kupata majibu, nina maanisha sababu hasa zilizomsukuma Rais kumteua huyu jamaa kwenye Uwaziri.

Angalizo: Sitaki atukanwe au adhalilishwe, nimeuliza hili kwa Maslahi Mapana ya Taifa

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom