Rais Samia aunda Wizara Mpya na kufanya Mabadiliko ya kimuundo baadhi ya Wizara. Amteua Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri

Rais Samia aunda Wizara Mpya na kufanya Mabadiliko ya kimuundo baadhi ya Wizara. Amteua Profesa Kitila Mkumbo kuwa Waziri

NILISEMA WAPIGA DEBE WA SAKATA LA BANDARI KULAMBA TEUZI SUBIRI WAKINA ZEMBWELA NA KITENGE KULAMBA UDC
 
DKT. ASHATU KIJAJI ATEULIWA KUWA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Miundo ya Wizara ambapo ameunda Wizara ya Viwanda na Biashara na amemteua aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Itakumbukwa Dkt. Kijaji alikuwa ni Waziri anayeshughulikia Viwanda, Biashara na Uwekezaji lakini kutokana na kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala ya uwekezaji Ofisi ya Rais sasa anabaki kuwa Waziri anayesimamia Viwanda na Biashara pekee huku Uwekezaji ukiunganishwa na Mipango na Waziri wake ni Prof. Kitila Mkumbo ambaye ameteuliwa na Rais Samia hii leo.

Rais Samia amemteua pia Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa, kabla ya uteuzi huu Mafuru alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi).

Rais Samia amemteua pia Elijah Mwandumbya kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi), kabla ya uteuzi huu Mwandumbya alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango.


Dkt.-Ashatu-Kijaji.jpg
IMG_0732.JPG
Dk.-Ashatu-Kijaji.jpg
Dmza6rFX0AAYY2O.jpg
 
Dar es salaam wamepata waziri wa kufutia machozi.

Ingawa hii game ipo so confusing. Yaani ipo hivi, huko majimboni ni wakaazi wachache wa Majinbo hayo waliofanikiwa kupata ubunge. Hivyo Dar es salaam inawacheka wakaazi wa majimbo kwamba hawana Dar ndiyo inawapatia wabunge.

Wakaazi hao wa Dar wakishapata ubunge, na kupewa uwaziri, wa majimboni wanawacheka wana Dar es salaam kuwa hawajatoa waziri.
 
Kuendelea kugawana keki ya Taifa, vijana jitajidini mjiajiri inalipa sana
 
Nchi isiyowekeza kwenye R&D, itaendelea kuburuzwa hadi kiama...

Nchi inayotegemea siasa na wanasiasa kuleta mapinduzi ya kiuchumi au maendeleo ya kiuchumi, itaendelea kuburuzwa hadi kiama...

Nchi inayotegemea wajenzi wa nchi wawe ni wageni na sio wazawa, itaendelea kuburuzwa hadi kiama...
 
Back
Top Bottom