HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 70,791
- 98,334
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Aidha, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha kuwa Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina tarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.
Vile vile, Mhe. Rais ameelekeza kuwa watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.
Pia, soma: Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya