Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Wale ndugu almaarufu "stupid people" mambo iko huku:

View attachment 2582521

Kwa aliyetajwa na CAG sasa ni suala la muda tu.

Aungurumapo simba mcheza nani?
Nisipompongeza Rais kwa hatua hii aliyoichukua nitakuwa mnafiki.

Naamini kama ana uchungu na dhamana tuliyompa kwa kiapo atahakikisha serikali inarecover kwenye loss zilizotokea.

Najua amewaambia Makatibu wakuu kuchukua hatua lakini ni mtego kwao kwani sehemu kubwa ya upigaji ni connection

Kuna watu wanapokea unsolistcated money somewhere safe
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri?

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, sioni jipya.
Mkuu sikubalian na wewe kwenye hili.
Jambo hili bado lipo mikononi mwa Rais kwa kias kikubwa...soma vizur hapo.. amemwelekeza "Katibu Mkuu Kiongozi"...huu ndo utawala wa kisheria unavyotaka mkuu.
Mpaka Hapo hamna shaka Mkuu labda useme katibu Mkuu Kiongozi hajiwezi au labda kama na yeye ni mtuhumiwa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Tumpe muda basi jamani....Na yeye si anaipitia kwa level yake? Kisha kama ambavyo hao watachukua hatua kwa wachini wao na yeye atachukua hatua kwa wale walio chini yake....Mimi naona Mh. Rais anachukua hatua kwakufuata sheria, kanuni na taratibu na ndiyo good governance hii....

Ameonyesha utulivu na anazingatia utawala wa sheria....
 
Mkuu sikubalian na wewe kwenye hili.
Jambo hili bado lipo mikononi mwa Rais kwa kias kikubwa...soma vizur hapo.. amemwelekeza "Katibu Mkuu Kiongozi"...huu ndo utawala wa kisheria unavyotaka mkuu.
Mpaka Hapo hamna shaka Mkuu labda useme katibu Mkuu Kiongozi hajiwezi au labda kama na yeye ni mtuhumiwa.
Umewaza sawa na mimi...
 
Wale ndugu almaarufu "stupid people" mambo iko huku:

View attachment 2582521

Kwa aliyetajwa na CAG sasa ni suala la muda tu.

Aungurumapo simba mcheza nani?

Pamoja na tangazo hili, mimi natamani kusikia/kuona ni nini kitatokea. Nataka kuona Rais atachukua hatua gani. Imekuwa ni mazoea kuona CAG anatoa ripoti na kutoa mapendekezo ni nini cha kufanya, lakini hatua hizo hazifanyiwi kazi, na kama zikifanyiwa, basi kuna watu wanatolewa kafara, na wale walengwa wwanabaki wakila nchi na kuppanga mipango ya kuendele kuiibia nchi. Si ajabu taasisi fulani ilisha tajwa mara nyingi katika ripoti za CAG lakini wahusika bado wapo tu kweny nafasi zao au pia wamepandishwa vyeo.
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?

Yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe wakiwemo mawaziri?

Alichokifanya Rais hapo ni sawa na kufunika kombe mwanaharamu apite, sioni jipya.
Mkuu ulitaka afanye nini ? Huyu huwa hakurupuki kama meko
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Nadhani ifike wakati serikali iondoe ajira za kudumu
Bado haitakuwa suluhisho.
Moja ya suluhisho kubwa ni kumpunguzia rais madaraka makubwa aliyonayo ikiwemo madaraka ya kuteua ma CEOs karibu wote. Madaraka haya yapunguzwe yapelekwe bungeni na kwenye mhimili wa mahakama....maana yake hapo ni katiba mpya.
 
Back
Top Bottom