Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Hatua nzuri,hii ni sawa na ile mmekutwa darasani mnapiga kelele halafu mwalimu anawaambia mchapane fimbo,na asiyemchapa fimbo mwenzake kisawasawa mwalimu anamchapa yeye mwenyewe,nawaona makatibu wakuu hapo vijasho vinawatiririka, hiyo ndio kazi mliokuwa mnaishangilia fanyeni kazi sasa ...
 
Teh Teh kwa hiyo sasa mnataka kutuambia kumbe CAG huwa anaonea watu? Vipi CAG hakuonea watu kwenye report ya miaka miwili iliyopita?😂😂😂😂😂
Umewahi sikia CAG kataja jina la mtu? Miaka hiyo iliyopita kwanza sijawahi sikia hatua yeyote imechukuliwa mfano pale BoT waliteketeza noti bandia za uongo.
 
Kazi imeanza......

, naamini safari hii hakuna atakaye salimika kama tu amehusika either moja kwa moja or indirect, au kazembea kutimiza wajibu wake au makosa yamefanywa na walio chini yake.
Bado sana tunaingia kuchukua mzigo tunatoka bila mzigo eti funguo hatuzioni!
 
Uwe na subira unakimbilia wapi...mbona unaongea Kama mzee wa fitina makazini huko..huu ni utawala wa sheria hawezi mtu kutumbuliwa tu bila kujiridhisha na kuhusika kwake kwenye ufisadi... mwingine ni waziri lakini alishitaki mwenendo mbaya wa taass au shirika ambalo lipo ndani ya wizara yake je unataka nae afukuzwe kwa kosa lipi?
Kumbe tuna mashaka na report ya CAG? Hayo mashaka ni kuanzia mwaka huu? Au na miaka iliyopita? Kumbe CAG anaweza kuwa alikuwa anawaonea watu au amesema uongo hivyo Rais anataka ajiridhishe kama aliyo yasema ni ya kweli au lah?😂😂😂😂! Kumbe hatupaswi kuwatukana wala kusema vibaya walio kuwa wanampiga CAG Au kuwa na mashaka nae?

Kumbe CAG haaminiki ndio maana rais lazima ajiridhishe kwanza teh teh
 
Hatua nzuri,hii ni sawa na ile mmekutwa darasani mnapiga kelele halafu mwalimu anawaambia mchapane fimbo,na asiyemchapa fimbo mwenzake kisawasawa mwalimu anamchapa yeye mwenyewe,nawaona makatibu wakuu hapo vijasho vinawatiririka, hiyo ndio kazi mliokuwa mnaishangilia fanyeni kazi sasa ...
Yani hapo ni mtego kwa makatibu wakuu lazima wawe Moto kwasabu wakizingua tu nao wanalimwa
 
Umewahi sikia CAG kataja jina la mtu? Miaka hiyo iliyopita kwanza sijawahi sikia hatua yeyote imechukuliwa mfano pale BoT waliteketeza noti bandia za uongo.
Kumbe hatutaki kuchukua hatua kwakuwa miaka iliyopita hazikuchukuliwa hatua? 😂😂😂😂😂vichekesho hakika
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe? yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe?
Kaachia sheria imewachukulie hatua ?....ulitakaje wewe ?
 
Kumbe tuna mashaka na report ya CAG? Hayo mashaka ni kuanzia mwaka huu? Au na miaka iliyopita? Kumbe CAG anaweza kuwa alikuwa anawaonea watu au amesema uongo hivyo Rais anataka ajiridhishe kama aliyo yasema ni ya kweli au lah?😂😂😂😂! Kumbe hatupaswi kuwatukana wala kusema vibaya walio kuwa wanampiga CAG Au kuwa na mashaka nae?

Kumbe CAG haaminiki ndio maana rais lazima ajiridhishe kwanza teh teh
Umeelewa lakini nilichosema mbona unaongea Kama umefunguliwa kutoka kwenye maporomoko, hebu soma uelewe syo unaparamia tu mambo
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Toka Maktaba :

17 February 2023

BODI MPYA YA WAKURUGENZI TRC, WATANZANIA WAWE WAVUMILIVU NA MRADI WA SGR

PROF. KONDORO ATAMBULISHA WAJUMBE WAPYA BODI YA WAKURUGENZI TRC

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania Prof. John Wajanga Kondoro akiwa na wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi TRC waliotambulishwa Bw. Benjamini Adam Mbimbi, Bw. Kondo Abdalah Kibugula, Bw. Joseph Elias Salema, Bw. Juma Samhando Kijavara na Bw. Peter Mayunga Noni wakipata maelezo

Habari kwa urefu :

17 February 2023
Dar es Salaam, Tanzania

WAJUMBE WAPYA WA BODI YA TRC WATEMBELEA SGR DAR-MORO, MWENYEKITI ANENA, MAENDELEO NA UJIO WA VIFAA. PIA WATANZANIA WAWE NA SUBIRA NA IMANI JUU YA MRADI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania – TRC Prof. John Wajanga Kondoro ametambulisha wajumbe wapya wa bodi ya wakurugenzi TRC na kuwaaga wajumbe waliomaliza muda wao katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya makao makuu TRC jijini Dar es Salaam, Februari 2023.

Wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi TRC waliotambulishwa ni Bw. Benjamini Adam Mbimbi, Bw. Kondo Abdalah Kibugula, Bw. Joseph Elias Salema, Bw. Juma Samhando Kijavara na Bw. Peter Mayunga Noni.

Wajumbe waliomaliza muda wao ni Bw. Wolfgang Ephraim Salia, Bi. Consolata Chrisostom Ngimbwa, Bw. Karim Godfrey Mattaka, Bw. Rogatus Hussein Mativila na Bw. Mahamud Mashaka Mabuyu.

Mwenyekiti wa Bodi Prof. Kondoro kwa niaba ya uongozi wa TRC amewashukuru wajumbe waliomaliza muda wao kwa mchango waliotoa kipindi chote walichokuwa katika nafasi za ujumbe na kuliwezesha Shirika kupiga hatua na kuongeza ufanisi katika utendaji wa Shirika.

“Lengo la kukutana hapa ni kutambuana na kutambua mchango wa wajumbe ambao wamelitumikia Shirika la Reli, waliingia katika kipindi ambacho tulikuwa kwenye sekeseke kuhusu maendeleo ya mradi wa SGR na mpaka tulipofika hapa, kwahiyo ni vyema kutambua mchango wao lakini pia kuwashukuru na kuwakaribisha wajumbe wapya” alisema Prof. Kondoro

Wajumbe wanaoendelea na nafasi zao ni pamoja na Bw. Jabir Bakari na Bi Lilian Ngilangwa. Baadhi ya wajumbe waliomaliza muda wao walipata fursa ya kutoa neno kwa menejimenti ya Shirika na kupongeza jitihada kubwa zilizofanywa kuhakikisha watumishi wanafanya kazi kwa weledi na kuleta tija katika utendaji wa Shirika.

“Nataka niwapongeze sana menejimenti hususani Mkurugenzi Mkuu, tunashukuru kwamba mradi unaendelea na vipande vyote vina wakandarasi, awali niliona menejimenti ni ndogo lakini nikupongeze Mwenyekiti kwa kuboresha muundo wa Shirika” alisema Bi. Consolata

Aidha, wajumbe wapya wamepata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma kwa lengo la kufahamu namna mradi wa SGR unavyotekelezwa na Shirika la Reli Tanzania.

“Lengo la ziara ni kwamba tumepata wajumbe wapya wa bodi, hivyo ni vizuri kuwapitisha wakajua mifumo na miundombinu watakayokuwa wanaisimamia ikiwemo hii SGR, hii ni sehemu ndogo tu lakini wakati mwingine watapata kutembelea maeneo mengine” alisema Prof. Kondoro.
Sources : TRC RELI TV / Mwanzo | TRC
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe? yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe?
Ulitaka afanyaje tumia akili
 
Hallo hapo kidogo samia umeonesha umuimu wa CAG mana aiwezekani sasa mireport inatoka kila leo watu wanakula kodi za wananchi kuanzia wao wakaguzi wanalipwa pesa kufanya ukaguzi pia na wale wanaokaguliwa pia nao ukaguzi waonesha wanapiga pesa alafu hyo output ya ukaguzi isifanyiwe kazi hapo wa tz tulikua tunakuona na wewe raisi ni mwizi tu
 
Mbuzi wa Kafala wamechacha . Ametafutwa sungura wa kafala Haaa.

Akina Mashimba Ndaki mbuzi wa kafala, Kabudi mbuzi wa Kafala, Lukuvi mbuzi wa kafala. Haaa.
January Makamba Mbuzi wa kufugwa hawezi chinjwa, Makame Mbarawa mbuzi wa kufugwa haitaiweje hawezi kuchinjwa, Napee je Vp kuhusu Ummy Mwalimu,

je kuna inawezekana MKRISTO akawa mbuzi wa kufugwa? haaa, et nani......... mataje
Mtaendelea kuumbuka kwa kudra za Mungu na udini wenu huo mpaka basi!
 
Kwahili tukio alilolifanya Mh Rais, Kuna watu tayari washamalizwa kisiasa..hawana hoja Tena🤣
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe? yeye kama Rais anachukua hatua gani kwa hao wakuu waliosimamia huo uzembe?
Ndo hatua zimeanza kuchukuliwa sasa mkuu, kwani mtaka raisi awafuate akawanyonge??

Baadhi yenu mnaidai katiba mpya ilhali hata hii iliyopo nyie tu mnashindwa kuifata.

Lazima afate protokali hawezi kuamka tu na kuwasweka ndani ndgu nao ni raia wa tz na ni binadamu wenye haki zao,
 
Ndio mamlaka zao za nidhamu/uwajibikaji..so kwa hili Mh Rais yupo sahihi
Kwa hiyo hao viongozi wa mashirika wana wajibishwa na nani? Kama wao wameelekezwa wawachukulie hatua wa chini yao….wao wana wajibishwa na nani? Katibu kiongozi? Rais hana imani na CAG? Hahahaha kwanini asiwachukulie hatua za kuwwaweka pembeni watu ambao wako kwenye mamlaka yake? Kwanini ana kwepa majukumu yake? CAG amesema uongo?
 
Nampongeza mno kwa hili, binafsi sikutegemea hata kama anaweza kunyanyua ukucha. Sikumdharau ila kwa jinsi huu utawala ulivyoshabihiana na ule wa janjajanja Jakaya, kwakweli sikutegemea hili.
 
Kumbe hatutaki kuchukua hatua kwakuwa miaka iliyopita hazikuchukuliwa hatua? 😂😂😂😂😂vichekesho hakika
Saizi zimeanza kuchukuliwa kwani hujaskia breaking news huko?

Kama hazitoshi Hilo ni suala jingine
 
Kwa hiyo hao viongozi wa mashirika wana wajibishwa na nani? Kama wao wameelekezwa wawachukulie hatua wa chini yao….wao wana wajibishwa na nani? Katibu kiongozi? Rais hana imani na CAG? Hahahaha kwanini asiwachukulie hatua za kuwwaweka pembeni watu ambao wako kwenye mamlaka yake? Kwanini ana kwepa majukumu yake? CAG amesema uongo?
Tukubali kujifunza kwa wengine pia, kujua kwingi ni hasara!
 
Back
Top Bottom