Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa Wakala wa Ndege za Serikali. Aagiza wabadhirifu washughulikiwe

Huyo ndio mhusika mkuu, TGFA ndiye mnunuzi kwa niaba ya serikali, ndege zinaponunuliwa anasaini yeye upande mmoja na mtendaji wa ATCL upande mwingine.
Sasa kama ni hivyo hiyo bodi na mtendaji wa ATCL mbona hawajawajibika!! Na je kufukuzwa kazi kwa hawa kutafuta ongezeko la malipo kwenye ile invoice ya pili?
 
Binafsi naona siyo sawa. Wanaweza wakalindana. Namuomba mhe. Rais Samia pamoja na kuwapa hiyo kazi lkn na yeye afuatilie kwa makini sana
Hata mimi naona sio poa! Mfano Masanja Kadogosa kama alihusika inamaana Katibu wake wa wizara ya ujenzi ndo atamwajibisha na kupeleka taarifa kwenye mamlaka za uteuzi!
Some thing wrong some where!
 
Mmmm kama kukwepa majukumu hivi! Kuna mtu hataki lawama hapa!
Wakurungenzi na makatibu wakuu ndi wezi sana wa hizi pesa tena wachunguzane wao kwa wao?
Ndo hapo haiwezekani maana wao ndo wameshika stream kubwa ya upigaji kama ingekuwa wa Chin basi mda sana washawatimua ..
 
Wengi tunam underestimate SSH lakini ni mkali hata kuliko 'makufuli'
 
Ndo hapo haiwezekani maana wao ndo wameshika stream kubwa ya upigaji kama ingekuwa wa Chin basi mda sana washawatimua ..
Jamani hapa hakuna jipya yale yale ya miaka yote!
Watu wataendelea kuiba kwa na kushirikia na jamaa zao ili wasichomane over!
 
Sasa kama ni hivyo hiyo bodi na mtendaji wa ATCL mbona hawajawajibika!! Na je kufukuzwa kazi kwa hawa kutafuta ongezeko la malipo kwenye ile invoice ya pili?
Invoice za malipo zinawahusu TGFA wao ndio wanaomkabidhi ndege ATCL kwa niaba ya serikali, kwani yenyewe haifanyi biashara za ndege.

ATCL ni mwendeshaji tu sio mnunuzi wa ndege wa moja kwa moja kutoka kwa wauzaji.
 
Washauri wa MAMA ndiyo wanaompotosha,japo simaanishi mama anakubali tu,bila kurizoni
 
Kama ATCL management hawahusiki, inakuwaje wanakuwa co-signatories kwenye manunuzi?
Hawana title hiyo kaka, TGFA anasign na bosi wa ATCL kumkabidhi ndege baada ya wao kuwa wameshazinunua. ATCL hana mawasiliano ya moja kwa moja na mtengenezaji wa ndege.
 
Washauri wa MAMA ndiyo wanaompotosha,japo simaanishi mama anakubali tu,bila kurizoni
Daaah kuna maamzi yanafanyika unajiuliza hivi kweli kuna kiongozi wa nchi hii?
Yaani honestly hapa report ya TAKUKURU ukiisikia ni ujinga ujinga tu lakini bado kiongozi anaisifia!
 
Rais ana akili huyu, ametanguliza mgambo believe maelekezo yote yanatoka kwake.
Yeye atakua anasema, katibu funga jera huyo.!!
Uongozi ni technical.
Mimi nadhani Makatibu wenyewe ni watuhumiwa( wafanyakazi wa serikali), Sasa watajichunguzaje kisha watoe majibu? Hili agizo linaonyesha Nia njema aliyonayo Mama yetu Rais ya kukomesha ubadhirlifu wa Mali za umma, lakini halitoi mwanga mzuri kumshughulikia tatizo! Kutakuwa na kuoneana.

Napendekeza
===
Watuhumiwa wote wa nafasi za kisiasa na kiutendaji serikalini kwenye sakata hili la upotevu wa fedha/ na ufujaji wa Mali za umma wangewekwa pembeni. Taasisi za Uchunguzi , ama TAKUKURU wakisaidiana na TISS ndiyo wangefanya kazi hiyo na kumpa Mama majibu kisha watu hao wakapelekwa kwenye vyombo vya sheria kwa mujibu ya mikataba ya kazi zao, miongozo ya maadili ya Utumishi wa umma. Na sheria nyingine za nchi yetu endapo wangekutwa na hatia.

Hatuhitaji kuunda tume ya Uchunguzi, hawa hawa walioajilia kwa kazi za kuchunguza na kudhibiti ndiyo wafanye kazi hiyo ya kubaini waliofuja Mali za umma.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Aidha, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amemuelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuhakikisha kuwa Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina tarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao.

Vile vile, Mhe. Rais ameelekeza kuwa watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhirifu wachukuliwe hatua za kisheria.

View attachment 2582469
Asiwaache wanasiasa wenzake ambao wizara zao zimetajwa na CAG.

Kula vichwa wote mawaziri uchwara
 
Limeshapita hilo, tusubirie report ya mwakani tena watu wale wale na mambo yale yale.
 
Huyo ndio mhusika mkuu, TGFA ndiye mnunuzi kwa niaba ya serikali, ndege zinaponunuliwa anasaini yeye upande mmoja na mtendaji wa ATCL upande mwingine.
Haya ni maneno yako bwana Philipo kuwa" Ndege zinaponunuliwa anasaini yeye upande mmoja na mtendaji wa ATCL upande mwingine" na hiyo ndiyo maana ya co-signatories!! Sio kuwa ATCL management wanasign wanapokabidhiwa ndege!!
 
Muda ndio utatupa jibu kama hii ni hadaa au kweli Mama yuko serious.
 
Haya ni maneno yako bwana Philipo kuwa" Ndege zinaponunuliwa anasaini yeye upande mmoja na mtendaji wa ATCL upande mwingine" na hiyo ndiyo maana ya co-signatories!! Sio kuwa ATCL management wanasign wanapokabidhiwa ndege!!
Anayehusika moja kwa moja na ile over invoicing aliyoisema rais pale ikulu ni TGAF sio ATCL, elewa hivyo mkuu Bulesi.
 
Inashangaza sana, kwanini Rais anawaagiza makatibu wakuu na watendaji wakuu wahakikishe wanapitia ripoti na kuwawajibisha wale waliohusika na uzembe?
Kwa uelewa wangu kiduchu, wenyewe hao wakurugenzi na Makatibu ni watuhumiwa ( rejea Aya ya mwisho ya taarifa).
 
Back
Top Bottom